Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

DKT SHEIN: Nchi Za Sadc Tutoe Kipaumbele Kwa Bidhaa

Posted on: August 8th, 2019

Na Mwandishi Wetu, MAELEZO

RAIS wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein amezitaka Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuweka mkazo wa matumizi ya bidhaa zake  na wataalamu wake wa ndani katika kutengeneza fursa za ajira na masoko ndani ya ukanda huo ili kukuza sekta za viwanda na biashara ndani ya jumuiya hiyo.

Akizungumza katika hafla ya kufunga Maadhimisho na Maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda katika Nchi za SADC leo Alhamisi (Agosti 8, 2019) Jijini Dar es Salaam, Rais Shein alisema umefika wakati kwa mataifa hayo kuzalisha bidhaa bora zenye kuweza kuleta ushindani katika masoko ya ndani na nje ya Jumuiya hiyo.

Dkt. Shein alisema Mataifa ya SADC hayana budi kutumia fursa ya maonesho hayo katika kutangaza fursa za ujuzi na ubunifu  kwa kuzalisha na kutengeneza mtandao wa imara wa mawasiliano baina ya Nchi hizo na kuweza kuwa na soko la pamoja litakalowawezesha kutengeneza fursa za ajira kwa wananchi wa Mataifa hayo.

Kwa mujibu wa Dkt. Shein aliongeza kuwa ili kufikia malengo ya uzalishaji wa bidhaa bora za viwandani ni wajibu wa Serikali zote kutengeneza mtandao imara wa miundombonu ikiwemo matumizi ya tekonolojia ya habari na mawasiliano kwa kuunda mikakati ya pamoja ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Jumuiya hiyo uliolenga katika kuimarisha sekta ya viwanda ndani ya jumuiya hiyo.

“Hatujakataa mchango wa wataalamu na bidhaa za nje, lakini chako ni chako na mwenzako si chako, hivyo hakikunyima usikasirike, ni wakati wetu sasa kuweka mkazo katika kutegemea wataalamu wetu na teknolojia zetu katika uzalishaji wa bidhaa zetu” alisema Dkt. Shein.

Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Maafisa wa Kiwanda cha viatu cha  gereza  la Karanga (Moshi), kuhusu bidhaa zinazotengenezwa kwa ngozi, kushoto kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.Paramagamba Kabudi, maonesho hayo yamefungwa rasmi leo 08 Agosti, 2019.

Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Maafisa wa Kiwanda cha viatu cha  gereza  la Karanga (Moshi), kuhusu bidhaa zinazotengenezwa kwa ngozi, kushoto kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.Paramagamba Kabudi, maonesho hayo yamefungwa rasmi leo 08 Agosti, 2019.

Aliongeza kuwa Nchi za Jumuiya hiyo hazina budi kutumia fursa za Maonesho na midahalo mbalimbali ya wataalamu inayojadiliwa katika Mikutano ya Jumuiya hiyo ili kuweza kubaini changamoto na hatua mbalimbali zinazopaswa kuchukuliwa ili kuiwezesha jumuiya hiyo kupiga hatua kubwa za Maendeleo ikiwemo kutengeneza fursa za ajira kwa wananchi wake.

Akifafanua zaidi Dkt. Shein aliongeza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar zimekuwa zikichukua hatua mbalimbali katika uboreshaji wa miundombinu ya miradi ya Maendeleo ambayo imekuwa kichocheo kikubwa cha fursa za ajira kwa vijana sambamba na kutengeneza mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kushiriki katika uchumi wa viwanda.

Akitolea mfano, Dkt. Shein alitaja baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa (SGR), ujenzi wa viwanda  vikubwa, vya kati na vidogo ambavyo kwa pamoja vinaifanya Tanzania kuwa kielelezo cha mfano katika Nchi za SADC katika utekelezaji wa Ajenda ya Maendeleo ya Viwanda ndani ya Jumuiya hiyo.

Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa alisema maonesho hayo yamekuwa chachu na kipimo kwa Nchi za SADC kutekeleza ajenda yake ya Viwanda, kwa kuwa makundi mbalimbali ya wazalishaji, wafanyabiashara na watoa huduma wameonesha udhubutu wa kufikia malengo hayo katika Nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya Pamoja  na  Viongozi (SADC) na Mawaziri kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC,  kwenye  hafla ya kufunga maoneshoa ya wiki ya viwanda.

Aliongeza kuwa jumla ya washiriki 5352 walishiriki katika midahalo mbalimbali ikiwemo Nchi SADC 14, taasisi za umma 64, viwanda 64, taasisi za kifedha 35, ambazo zote kwa pamoja zilitoa uzoefu na kuweza kuongeza fursa ya masoko na kuweza kuimarisha mitandao ya mawasiliano baina yao.

Naye Waziri wa Habari, Utalii na Malikale wa Zanzibar,                 Mahmoud Thabit Kombo alisema ili kufikia malengo ya Mpango Mkakati wa Jumuiya hiyo, nchi za SADC hazina budi kutoa na kuweka mkazo wa ushiriki wa sekta binafsi katika ujenzi wa uchumi shirikishi, kwa kuwa ushirikiano baina ya sekta hiyo na serikali utawezesha kutengeneza fursa mbalimbali za kiuchumi katika mataifa hayo.

Naye Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo, Dkt. Stagomena Tax, aliisifu Serikali ya Tanzania kwa kuwa mfano ndani ya Jumuiya hiyo katika eneo la ujenzi wa uchumi wa viwanda, na hivyo kuzitaka nchi nyingine kuiga mfano huo ili kuweza kuleta mtangamano ndani ya Nchi wanachama.

Aliongeza kuwa ili kuweza kujenga uchumi jumuishi kwa wananchi ndani ya jumuiya hiyo, Sekretarieti ya jumuiya hiyo itaelekeza nguvu yake katika kuimarisha miundombinu ya usafiri wa bidhaa zilizopo ndani ya jumuiya hiyo, kwani bila miundombinu ya uhakika hakutoweza kuwa na mazingira wezeshi ya kuwasaidia wananchi ikiwemo kuondoa vikwazo vya kibiashara ndani ya jumuiya hiyo.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO