Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

JWTZ Wapewa Jukumu la Kulinda Ukuta Unaozunguza Migodi ya Tanzanite

Posted on: April 7th, 2018

Frank Mvungi, Maelezo Manyara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaasa watanzania kuendelea kushikamana katika mapambano ya kiuchumi yanayoongozwa na Serikali ya Awamu ya Tano kwa faida ya kizazi hiki na kijacho.

Kauli hiyo imeitoa leo wakati akizindua ukuta uliojengengwa kuzunguka eneo la migodi ya Tanzanite mirerani mkoani Manyara ikiwa ni moja ya hatua zinazochukuliwa na Serikali kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi yakiwemo madini  ya Tanzanite yanawanufaaisha wananchi wote na kuchochea ukuaji wa uchumi.

“ Wapo waliosema kuwa ujenzi wa ukuta huu hautawezekana lakini leo Jeshi letu limethibitisha kuwa  yanayowezekana ulaya hata sisi kama Taifa tukiamua tunaweza na kukamilika kwa ukuta huu ni kielelezo tosha” Alisisitiza Mhe. Rais  Dkt. Magufuli.

Akifafanua Rais Magufuli amesema kuwa Serikali itajenga miundo mbinu yote muhimu katika eneo ikiwemo barabara  ili kuchochea ukuaji wa biashaara ya madini ya Tanzanite ambapo kutakuwa na utaratibu rafiki kwa wachimbaji wote ili Serikali iweze kupata mapato stahiki na wachimbaji wanufaike.

Akitolea mfano Rais Magufuli amesema kati ya makampuni 1700 ni makampuni 25 tu yaliyokuwa yakilipa kodi hali iliyochochea upotevu wa mapato ya Serikali kwa muada mrefu hali iliyozorotesha maendeleo katika eneo hilo na katika Taifa kwa ujumla.

“ Madini haya ni mali yetu hivyo ni lazima tuilinde kwa gharama yoyote na sasa nakuagiza mkuu wa majeshi (CDF) kuanzia sasa ukuta huu utalindwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na sio SUMA  JKT wala mtu mwingine yoyote” Alibainisha Dkt. Magufuli.

Katika eneo hili kutakuwa na Kituo cha pamoja cha kutolea huduma, mabenki na huduma zote zitakowezesha wafanyabiashara kushiriki kikamilifu katika uzalishaji na uuzaji wa madini hayo kwa kuwa mnada wa madini hayo utakuwa ukufanyika katika eneo hilo la mirerani na si kwingineko kama ilivyokuwa awali.

“ Tunapozuia wizi wa Tanzanite, dhahabu, wizi wa wanyama wetu, wahusika hawawezi kufurahia na hawa ni watu wenye uwezo mkubwa hivyo uzalendo katika kulinda rasilimali zetu ndio utakaosadia kama vijana walioshiriki kujenga ukuta walivyoonyesha mfano wa uzalendo wao kwa vitendo kwa kushiriki katika ujenzi wa ukuta huu” Alisema Dkt. Magufuli na kusisitiza.

Pia Rais Dkt. Magufuli alimpongeza mgunduzi wa madini ya Tanzanite mzee Jumanne Ngoma na kutoa shilingi milioni mia moja kwa ajili ya matibabu kwa mgunduzi huyo ikiwa ni ishara yakutambua mchango wake katika maendeleo ya Taifa kufuatia ugunduzi huo alioufanya mwaka 1967 katika eneo la mirerani.

Mkoa wa Manyara umeshapokea zaidi bilioni 6 kwa ajili ya mpango wa elimu bure na pia kuna miradi ya upanuzi wa vituo vya afya, zahanati na mwaka huu wa fedha zaidi ya Bilioni 1.6 zimetwngwa kwa ajili ya ujenzi wa hosipitali ya  rufaa ya mkoa, utekelezaji wa miradi ya maji yenye thamani  ya zaidi ya bilioni 2.4 katika eneo la mirerani unaendelea na wilaya ya Simanjiro kwa ujumla ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuondoa adha ya upatikanaji wa maji.

Kwa upande wake Waziri wa Madini Anjellah Kairuki amesema kuwa Serikali kupitia Wizara yake imeshaandaa kanuni zitakazosimamia uendeshaji wa eneo hilo lenye ukuta wa kuzunguka migodi ya Tanzanite ili dhamira ya kujengwa kwa ukuta huo itime.

“ Tayari katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita tumeona tofauti ya makusanyo ya mapato yanayotokana na madini ya Tanzanite ukilinganisha na miakaliyopita ambapo kwa miezi mitatu tumekusanya zaidi ya milini mia saba” Alisisitiza Kairuki.

Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi amesema kuwa muda uliopangwa katika kutekeleza mradi huo ni miezi sita ambapo kutokana na umahiri na uwezo wa Jeshi mradi huo umetekelezwa kwa miezi mitatu tu.

Ujenzi wa ukuta huo ni Agizo la Rais Dkt. John Magufuli alilolitoa mwezi Novemba mwaka 2017 wakati akizindua barabara ya KIA  mererani iliyojengwa kwa kiwango cha lami, vijana zaidi ya 2000 wameshiriki katika ujenzi wa ukuta huo wakiwa ni wale wa operesheni Magufuli na Operesheni Kikwete ambao wameonyesha uzalendo wa hali ya juu kwa vitendo.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO