Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Majaliwa: Viwanda vimepunguza tatizo la Ajira kwa Vijana

Posted on: October 7th, 2018

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema changamoto ya upatikanaji wa ajira hususani kwa vijana imeanza kupungua nchini baada ya viwanda vingi kuanza kufanya kazi.

Aliyasema hayo Jumamosi, Oktoba 6, 2018 alipotembelea kiwanda cha kukoboa kahawa cha BUKOP na cha kusindika kahawa cha Tanica, mjini Bukoba.

Alisema kwa sasa tabia ya vijana wengi kukaa vijiweni imepungua kwenye maeneo mengi nchini baada ya wengi kuajiriwa katika viwanda mbalimbali vilivyoanzishwa na kufufuliwa.

Waziri Mkuu alisema viwanda vimekuwa vikitoa ajira nyingi kwa wananchi, ambapo alitolea mfano kiwanda kimoja cha Tanika kilichoajiri watumishi 800.

“Nyie mlioajiriwa kiwandani hapa hakikishe mnafanya kazi kwa bidii, weledi, uaminifu na uadilifu wa hali ya juu ili kukiwezesha kiwanda kuendelea na uzalishaji,” alisisitiza.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Kagera kwa ziara ya siku nne, inayolenga kufuatilia maendeleo ya viwanda na zao la kahawa, ambalo ni kati ya mazao makuu sita ya biashara.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Bw. Bernad Limbe kuhakikisha anatafuta eneo kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo.

Aliyasema hayo baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi waliokuwa wakifanya biashara katika eneo bandari na kuondolewa bila ya kupewa eneo lingine.

Waziri Mkuu alisema ni marufuku kuwaondoa wananchi katika maeneo yao ya kufanyia biashara bila ya kuwaonesha eneo lingine ambalo watalitumia kwa aliji ya kufanyia biashara zao.

Awali, Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Bw. Linus Leopord alisema kwa mwaka wanazalisha tani 600 za kahawa iliyokaangwa na kusagwa, ambayo inatosheleza kwa mahitaji ya soko.

Pia kiwanda cha kahawa cha Tanica kinauwezo wa kuzalisha kahawa ya unga tani 500 kwa mwaka ila kutokana na uchakavu wa miungombinu kinazalisha tani 300 kwa mwaka.

Kuhusu masoko Bw. Leopord alisema kwa sasa mauzo yameongezeka, wanauza tani 50 ya kahawa iliyokaangwa na kusagwa kwa mwezi, ambapo awali walikuwa wanauza tani 32.

Kadhalika, Meneja huyo alisema wameimarisha na kuongeza soko la nje ambapo kwa sasa wanauza tani 35 za kahawa ya unga kwa mwezi, awali walikuwa wanauza tani 20.

Alisema kiwanda cha Tanika kinamilikiwa na chama cha ushirika cha KCU (53.37 %), KDCU (31.8%), Hazina (7.67), TFC (6.22%) na wafanyakazi wa Tanica (0.92%).

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO