Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Majaliwa- Watumishi wa mipakani dhibitini Silaha

Posted on: September 23rd, 2017

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi katika mipaka mbalimbali nchini ukiwemo wa Namanga mkoani Arusha kuhakikisha wanachunguza kwa umakini mizigo yote inayoingia ili kudhibiti uingizwaji wa silaha na dawa za kulevya nchini.

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Septemba 21, 2017) alipotembelea kituo cha Pamoja cha Forodha cha Namanga wilayani Longido kilichopo kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya na kisha kuzungumza na wafanyabiashara ndogo ndogo.

Waziri Mkuu amesema ni vema watumishi wa vituo vya forodha katika maeneo ya mipaka wakawa makini kwa kuhakikisha wanadhibiti uingizwaji wa silaha pamoja na dawa za kulevya nchini kwa sababu ndiyo zinazotumika katika matukio ya kihalifu.

Pia Waziri Mkuu ameziagiza mamlaka mbalimbali zinazosimamia ubora wa bidhaa kwenye vituo vote vya Forodha nchini kuhakikisha wanachunguza bidhaa zote na kujiridhisha ubora wake kabla ya kuruhusu kuingizwa nchini na kutumika.

“Tusingependa nchi yetu kuwa eneo au shimbo la kutupia bidhaa zisizokuwa na ubora Wizara zote zinazohusika na udhibiti wa ubora wa bidhaa zihakikishe suala la ukaguzi wa viwango vya ubora wa bidhaa zote zinazoingia nchini linapewa kipaumbele.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Longido, Bw. Daniel Chongolo pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Bw. Juma Mhina kukutana na wananchi wanaofanya biashara ndogo ndogo katika eneo hilo pamoja na viongozi wa TRA na kuwatafutia eneo lingine kwa ajili ya kufanyia biashara zao.

Amesema kwa kuwa wananchi hao awali walikuwa wanafanya biashara zao ndani ya eneo hilo kabla ya kujengwa kituo hicho cha Pamoja cha Forodha, ambapo kwasasa hawaruhusiwi kutokana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya Tanzania na Kenya kuhusu uendeshaji wa kituo hicho hivyo ni vema wakawatafutia eneo jingine nje ya uzio wa kituo hicho.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO