Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

“Nchi Yetu iko Salama dhidi ya Corona” – Dkt. AbbasI

Posted on: March 15th, 2020


Na. Immaculate Makilika - MAELEZO

Serikali imesema nchi iko salama dhidi ya ugonjwa wa CORONA  na tayari imechukua hatua kadhaa za tahadhari ili kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo hapa nchini.

Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari leo jijini Dodoma, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa, Serikali imeendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha kwamba ugonjwa huo sio tu hauingii nchini, lakini pia kuzuia kusambaa kwa maambukizi endapo utaingia.

“Zipo hatua zinazochukuliwa ndani ya Taasisi na Wizara moja moja, lakini pia zipo hatua za kitaifa za kukabiliana na ugonjwa huu, na hivyo naomba kuwatoa hofu watanzania kuhusu ugonjwa huu” alisema Dkt. Abbasi

Akifafanua hatua ya kwanza ya kukabiliana na ugonjwa huo, Dkt. Abbasi alisema, Serikali imeandaa utaratibu maalum katika maeneo ya Viwanja vya  ndege na maeneo ya mipakani, ambapo watu hawapimwi ugonjwa  wa corona bali joto la mwili ili kuangalia endapo joto limezidi kiwango cha kawaida  cha binadamu.

“Watanzania waendelee kuchukua tahadhari kama Rais Magufuli alivyoeleza na wazingatie maelekezo ya namna ya kujikinga yanayoendelea kutolewa na Wizara ya Afya kupitia wataalamu  wake” alisema Msemaji wa Serikali

Dkt. Abbasi amefafanua kuwa  katika hatua ya pili, Serikali imeandaa  vituo maalum vya kuwatenga washukiwa, na kuna vifaa vyote vya kupima huu ugonjwa. Aidha, hatua ya tatu ni kuwepo kwa hospitali maalum katika kanda zote nchini, ambazo zimetengwa  na zitatangazwa endapo atatokea mgonjwa wa CORONA. 

Vilevile, Serikali inaendelea  kufanya jitihada  katika kupambana na ugonjwa huo  ikiwemo kusitisha safari za ndege katika nchi za China na Italia na safari ya timu ya Taifa ya mpira wa miguu iliyokuwa iende nchini Tunisia kwa ajili ya mchezo uliokuwa ufanyike hivi karibuni .

Dkt. Abbasi amevipongeza Vyombo vya Habari nchini kwa kuitikia wito wa Rais wa kuhabarisha umma kuhusu ugonjwa huu, na kuwataka kuzingatia maelekezo ya wataalamu.

 

Mwisho

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO