TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewasili Jijini Pretoria nchini Afrika Kusini ambapo hapo kesho tarehe 25 Mei, 2019 atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Afrika ya Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa.
Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Philip Mangula amewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oliver Tambo Jijini Johannesburg na kisha kuelekea Pretoria.
Rais Mteule Mhe. Cyril Ramaphosa ataapishwa kuwa Rais wa 5 wa Afrika Kusini katika sherehe zitakazofanyika katika uwanja wa Loftus Versfeld Jijini Pretoria.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Pretoria
24 Mei, 2019
Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO