Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Rais Magufuli awataka Watanzania kujivunia Mafanikio ya Nchi yao

Posted on: October 11th, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema Watanzania wana kila sababu ya kutangaza na kujivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi kifupi cha miaka minne iliyopita na ameahidi kuendelea kusimamia rasilimali za Taifa ili ziwanufaishe zaidi.

Mhe. Rais Magufuli ameyasema hayo  tarehe 10 Oktoba, 2019 wakati akihutubia wananchi wa Mkoa wa Katavi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Azimio Mjini Mpanda.

Amesema juhudi kubwa zilizofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano kubana mianya ya wizi, ufisadi, rushwa, matumizi mabaya ya ofisi na mali za umma na kudhibiti nidhamu kwa watumishi wa umma zimesaidia kuokoa fedha nyingi ambazo zimetumika kutekeleza miradi mingi ya maendeleo ikiwemo ile ambayo ilionekana kutowezekana.

Mhe. Rais Magufuli ametaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Nyerere ambao utagharimu shilingi Trilioni 6.5, ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge railway – SGR) utakaogharimu shilingi Trilioni 7.2, ununuzi wa ndege, ujenzi wa barabara na madaraja makubwa, ujenzi wa vituo vya afya na Hospitali za Wilaya, ujenzi wa miundombinu ya elimu na kutoa shilingi Bilioni 23.8 kila mwezi kwa ajili ya kugharamia elimu bila malipo kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

“Ni lazima tujiulize maswali sisi Watanzania bila uoga na bila kumuonea mtu, kama tumeongeza ukusanyaji mapato kutoka Bilioni 850 hadi Trilioni 1.3 na mwezi uliopita tumekusanya shilingi Trilioni 1.7, kama tumejenga Vituo vya Afya 352 kwa mpigo, tumejenga Hospitali za Wilaya 69 wakati tangu tupate uhuru tulikuwa na Hospitali za Wilaya 77 tu, hela hizo zilikuwa zinakwenda wapi? Ukweli unabaki palepale, kama tumenunua ndege na sasa zitakuwa 11 kwa nini hatukununua miaka 50 iliyopita? Nyerere alipoondoka aliacha ndege, zote zimepotea, zipo wapi? Hilo nalo ukisema ni nongwa ndugu zangu, ukitaka kupima maendeleo ni lazima ujue mahali ulipotoka, mahali ulipo na mahali unapokwenda, hicho ndicho kipimo cha maendeleo cha kila mtu, treni ilikua inakufa mpaka tukabinafsisha kwa watu wengine, hapa Mpanda mlikuwa hamuoni treni, leo treni inakuja, ndugu zangu mnasahau? Amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Amewataka viongozi wote wa Serikali, siasa, Dini na taasisi binafsi kuyatangaza mafanikio hayo makubwa ili Watanzania wajue nchi yao inakokwenda na wapate moyo zaidi wa kuendelea kuijenga kwa kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa.

Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Homera kwa juhudi kubwa alizozifanya kusimamia maendeleo ya Mkoa huo katika kipindi kifupi cha miezi 4 tangu ateuliwe kuongoza Mkoa huo ambapo amefanikiwa kusimamia uanzishaji wa soko la madini na hivyo kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka shilingi laki 6 kwa mwezi hadi kufikia shilingi Milioni 148, kusimamia masoko ya mazao ya tumbaku, pamba na mahindi, kutatua kero za wananchi ikiwemo migogoro ya ardhi na mkakati wa kuanzisha viwanda.

Mhe. Rais Magufuli ameahidi kuwa Serikali itatoa fedha za kujenga kiwanda cha kuchambua pamba (Ginnery) katika Mkoa wa Katavi ambacho kitagharimu shilingi Bilioni 1.6 lakini amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Wizara ya Kilimo kuhakikisha wakulima wa pamba ambao hawajapata malipo ya kilo Milioni 6 za pamba wanalipwa ndani ya siku 7.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Maji na Mkoa wa Katavi kufuatilia miradi ya maji ambayo utekelezaji wake unasuasua Mkoani humo ikiwemo miradi 9 yenye thamani ya shilingi Bilioni 3.109.

Mhe. Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa na taarifa baadhi ya wakimbizi wa kutoka nchi jirani wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu Mkoani Katavi na ametoa wito kwa wakimbizi hao kuacha vitendo hivyo na Vyombo vya Dola kuhakikisha uhalifu huo unakomeshwa.

Kabla ya mkutano huo, Mhe. Rais Magufuli amefungua barabara ya lami ya Sitalike – Mpanda yenye urefu wa kilometa 36.9 ambayo imegharimu shilingi Bilioni 39.8 (fedha zote zimetolewa na Serikali ya Tanzania) na pia ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Tabora (Usesula) – Konga – Mpanda yenye urefu wa kilometa 342.9 ambayo itakapokamilika Machi 2021 itagharimu shilingi Bilioni 450.

Pia Mhe. Rais Magufuli amefungua Kituo Kikuu cha Mabasi cha Mkoa wa Katavi kiitwacho Mizengo Pinda, ambacho ujenzi wake umegharimu shilingi Bilioni 4.4 na amewapongeza wananchi wa Manispaa ya Mpanda kwa kupata kituo hicho pamoja na kujengewa barabara mpya za Mjini zenye urefu wa kilometa 7.7 kwa gharama ya shilingi Bilioni 8 hali inayoufanya Mji huo kuwa nadhifu.

Kesho tarehe 11 Oktoba, 2019 Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli ataendelea na ziara yake Mkoani Katavi ambapo ataweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilowati 132 kutoka Tabora kwenda Mpanda, ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Tanganyika na ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Mpanda – Vikonge.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO