Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

RAIS MAGUFULI: Tumieni Vifaa vya Wawekezaji wa Ndani

Posted on: September 16th, 2019

Na Paschal Dotto, MAELEZO

 RAIS Dkt. John Magufuli amewataka watendaji wanaosimamia miradi ya Serikali kutumia vifaa vinavyozalishwa na viwanda vya ndani ili kuinua sekta ya viwanda na kuongeza ajira kwa watanzania  wanaofanya kazi katika viwanda hivyo.

 

Akizungumza katika uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza mabomba ya plastiki cha Pipe Industirial Co.Ltdleo (Septemba 16, 2019) Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema kuwa Serikali inatekeleza miradi mingi mkubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, maji na sekta ya umwagiliaji ambayo yote hiyo inatumia mabomba ya kusafarisha maji.

 

“Miradi yote inayotekelezwa na Serikali inahitaji matumizi ya mabomba kwa asilimia 100, kwa hiyo ni lazima tutumie mabomba yanayotengenezwa nchini, sijasema tusiagize pengine lakini lazima tuwe wazalendo ili kuinua sekta yetu ya viwanda kwa kulinda viwanda vyetu vya vinavyozalisha bidhaa mbalimbali hapa nchini” alisema Rais Magufuli.

 

Rais Magufuli alisema kuwa viwanda vinavyojengwa nchini vitakuwa na faida nyinyi kwa wananchi na kwa Serikali kwa ujumla ikiwemo, upatikanaji wa ajira, ambapo Serikali itakusanya kodi ambazo zitatumika katika ujenzi wa barabara, ununuzi wa Ndege, ununuzi wa madawa, pamoja na uuzaji wa bidhaa zinazoenda nje zitakazoifanya Serikali kupata fedha za kigeni.

 

AIdha Rais Magufuli alisema katika kuhakikisha sekta ya Viwanda imekua, Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kufufua viwanda vuilivyokufa, kuondoa  urasmu katika taasisi zinazohusika na viwanda kama TBS, TFDA, NEMC, OSHA na Taasisi zinginezo ili kuwawezesha wawekezaji kuja kuwekeza kwa wingi nchini.

 

“Serikali imefanya yote hayo kwenye Taasisi husika, lakini pia imeweza kupunguza utitiri wa kodi kwa wafanyabiashara na kwa wenye viwanda, kwa mwaka huu wa fedha tumefuta tozo zipatazo 54 ambazo zingekuwa zinakwamisha juhudi za Serikali za kuwa na viwanda vya kutosha”, Rais Magufuli.

 

Rais Magufuli amesema kuwa kiwanda cha Pipe Industirial Co.Ltd Jijini Dar es Salaam ni kiwanda ambacho kinatumia teknolojia ya kisasa kuzalisha mabomba ambapo uwekezaji wake umetumia Bilioni 120 kwa wawekezaji kujenga kiwanda hicho.

 

“Nimefurahi kusikia kwamba wakati wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa kiwanda hiki watu wapatao 215 wamepata ajira, ambapo awamu ya pili itakapokamilika kiwanda hiki kitaweza kuzalisha mabomba ya kusafirisha gesi, mafuta na nyaya za umeme na kitaajili watu wapatao 500 hii ni hatua kubwa katika kutekeleza azma ya Serikali ya kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa kati wenye viwanda”, Rais Magufuli.

 

Aidha Rais Magufuli, alisema kuwa Sekta ya viwanda ni Sekta muhimu kwa nchi yoyote duniani, kwani Takwimu za Shirika la Biashara Duniani (WTO) zinaeleza kuwa asilimia 70 ya biashara ya kimataifa kwa mwaka 2018 bidhaa za viwandani zilichukua nafasi kubwa na kuwa na thamani ya dola za kimarekani Trilioni 12.41 ikifuatiwa na bidhaa ya mafuta asilimia 15, bidhaa za kilimo asilimia 10 na bidhaa nyinginezo asilimia 5 na thamani yake ni dola trilioni 5.

 

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa, alisema kuwa Serikali kupitia Wizara hiyo inalenga kuwasaidia wafanyabiashara kuzalisha kwa kulenga masoko yote ndani na nje ya nchi ili kuinua sekta hiyo muhimu nchini.

 

“Kiu ya Serikali ya Awamu ya Tano, ni kuona Tanzania hatuzalishi tu kwa soko la ndani, bali tunazalisha kwa ajili ya masoko ambayo Tanzania ni mwanachama wa jumuiya mbalimbali, kwa hiyo uzalishaji katika viwanda vyetu ni vizuri ukalenga masoko ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika(SADC) na Soko la Pamoja la Nchi Huru za Afrika (AU)”, Waziri Bashungwa.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO