Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Viongozi wa SADC Tanzania ni Nyumbani kwao- Dkt Abbasi

Posted on: August 8th, 2019

Na Pascal Dotto-Maelezo

Msemaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Hassan Abbasi amesema kuwa Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa  Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika- SADC kwa viongozi Tanzania ni nyumbani.

Akizungumza katika Kipindi cha 360 cha Clouds TV, Dkt. Abbasi amesema kuwa Tanzania ina historia kubwa kwa nchi za kusini mwa Afrika tokea enzi za ukombozi wa nchi hizo, ambapo Tanzania ilitumika kama kitovu cha wapigania uhuru.

“Viongozi hawa wengi wanarudi nyumbani, ikumbukwe kuwa Tanzania ndiyo ilikuwa moja kati ya mataifa matatu yaliyoasisi kamati ya Ukombozi ya Nchi za Kusini mwa Afrika, Tanzania ndiyo ilikuwa Makao Makuu ya ukombozi na  Ofisi Kuu ya ukombozi ipo Jijini Dar es Salaam, kwa hiyo hii ni hitoria kubwa kwa nchi yetu”, Dkt.Abbasi.

Dkt.Abbasi amesema kuwa Mkutano huu ambao ni fursa kwa watanzania maandalizi yake yamekamilika na sasa Tanzania ipo tayari kuwakaribisha wageni kutoka nchi wanachama wa SADC, huku baadhi ya mambo yakikamilishwa na kamati ya maandalizi kutoka SADC, Serikali ya Tanzania, wabia wa SADC pamoja na Sekta binafsi.

Aidha, Dkt. Abbasi amesema kuwa nchi za SADC zimekuwa na ajenda kubwa ya kutekeleza ujenzi na kuimarisha viwanda Jambo ambalo alisisitiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli wakati wa ufunguzi wa maonesho ya nne ya wiki ya viwanda ya Nchi wanachama wa SADC.

“Mhe.Rais Magufuli anaamini kwenye Sera ya Viwanda kama Tanzania tunavyotekeleza Sera hii, siyo kwa Tanzania tu bali hata kwenye nchi wananchama wa SADC. Rais  ata sukuma maendeleo ya viwanda kwani atakuwa Mwenyekiti wa SADC, na kama mnavyojua nchi wanachama wanatengeneza ajenda kuhusu ukuaji na uimarishaji wa viwanda”, Dkt.Abbasi.

Amesema kuwa viwanda ndiyo nguzo ya Maendeleo kwa nchi wanachama na kama Rais Magufuli, alivyosisitiza kuwa Afrika lazima ifanye biashara yenyewe kwa yenyewe badala ya kutegemea kufanya biashara na Nchi za Ulaya. Hivyo, SADC ni fursa kwa nchi wanachama kununua na kuuza bidhaa kwenye jumuia, kama nchi inahitaji mahindi basi Tanzania iuze mahindi yake ndani ya Jumuiya ili kukuza soko.

Dkt.Abbasi alisema kuwa Rais Magufuli amekuwa ni kiongozi ambaye anasimamia yale anayoyaamini ili kuwaletea Maendeleo wananchi wake kwa hiyo sasa atakwenda kusukuma utekelezaji wa ujenzi wa viwanda kwa nchi wanachama.

“Kuna mwanahistoria mmoja anaitwa Walter Rodney ambaye aliandika kitabu kushusu namna gani mataifa ya Ulaya yanayadidimiza mataifa ya Afrika, lakini pia unaona siku ile Rais anaongea na kukubaliana na msomi mwingine aliyeandika kuwa namna gani Afrika inajididimiza kwa hiyo msimamo wake utaifanya Tanzania na SADC kutekeleza ujenzi wa viwanda akiwa kama mwenyeketi wa Jumuiya hiyo kwa mwaka mmoja”, Dkt.Abbasi.

Dkt.Abbasi alisema kuwa nchi za SADC zinatakiwa kuwa na viwanda vya kuchaka malighafi na kuzalisha bidhaa ili kuongeza thamani, akitolea mfano wa mahindi ukiuza bila kuchakatwa hindi moja shilingi 200. Lakini kumbe likiwa limechatwa na kuzalisha unga unaweza ukauza kilo moja kwa shilingi  2,000, kwa hiyo ajenda ya kujenga viwanda vya kuchakata mazao itasimamiwa vema itakuza thamani ya bidhaa ndani na Nje ya Jumuiya.

Dkt. Abbasi alisema kuwa watanzania wengi sasa wameamka na Serikali ambacho inafanya ni kuwawezesha waamke na kuchangamkia fursa za biashara ndani ya SADC. Alitolea mfano kwenye maonesho ya SADC ambayo yanaendelea Jijini Dar es Salaam kuwa wapo watanzania ambao wanaonesha bidhaa zao wanazopeleka SADC.

“Takwimu zinaonesha watanzania tumeaka sana kwenye soko la SADC, tumepeleka bidhaa zinazofikia dola za kimarekani milioni 900 na tumengiza bidhaa zinazokadiriwa kufikia Dola milioni 600, kwa hiyo sisi bado kitakwimu tumechangamka zaidi kwenye soko la SADC.

Dkt.Abbasi alisema kuwa Serikali imeweka mikakati kwa Taasisi zinazohusisha masula ya biashara ikiwemo Tantrade na Bodi ya Masoko ya Mazao Mchanganyiko, kuitafuta masoko na kufanya utafiti ili kuwasaidia wafanyabiashara.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO