Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Wanaovujisha Mapato Uwanja wa Taifa Kuchukuliwa Hatua KalI

Posted on: March 15th, 2020


Na Mwandishi Wetu, Machi 15, 2020.

Serikali itawachukulia hatua kali  za kisheria wale wote watakaobainika kushiriki kuvujisha na upotevu wa mapato katika Uwanja wa Taifa na ule wa Uhuru Jijini Dar es Salaam wakati wa mechi za mpira wa miguu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma,  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji  Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema, pamoja na kuongezeka kwa mapato katika mechi ya Yanga na Simba iliyochezwa hizi karibuni katika Uwanja a Taifa kufikia shilingi Milioni 545.4/=, bado  Serikali imebaini mianya ya upotevu wa mapato katika uwanja huo.

“ Serikali inawaonya wale wote waliokuwa wanashiriki katika kuvujisha na kufanikisha upotevu  wa mapato wakati wa mechi katika Uwanja wa Taifa na ule wa Uhuru, na kwamba haitasita kuwachukulia hatua kali dhidi yao pale watakaobainika “.

Amesema,  Serikali inaendelea kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na uvujishaji na upotevu wa mapato katika viwanja hivyo ili kuziba mianya yote na tayari baadhi ya njia zinazotumika zimeshabainika.

Dkt. Abbasi amesema kwamba, kwa upande wa watendaji watakaobainika kujihusisha na uvujishaji na upotevu wa mapato, nao watachukuliwa hatua kali bila kujali nafasi zao na maeneo wanayosimamia wakati wa mechi zitakazofanyika katika viwanja hivyo.

Kutokana na kuongezeka kwa mapato ya mechi kati ya timu za Yanga na Simba , Serikali imepata mapato ya jumla ya shilingi milioni 153.2 tu. Hatua ya kudhibiti mianya ya uvujishaji na upotevu wa fedha za Serikali moja ya mikakati ya kuhakikisha kwamba Serikali inapata mapato yake sahihi kutoka katiuka vyanzo vyake. Mapato hayo ndiyo yanayoumika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo yenye lengo la kutatua kero za wananchi.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO