Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa asisitiza Mshikamano Kwa Watanzania

Posted on: October 9th, 2019

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kushikamana na wazingatie ujumbe wa mbio za mwenge za mwaka huu unaohimiza umuhimu wa maji, uchaguzi wa Serikali za mitaa, vita dhidi ya rushwa, malaria, UKIMWI na dawa za kulevya.

Ametoa wito huo leo asubuhi (Jumatano, Oktoba 9, 2019) wakati akizungumza na viongozi wa Halmashauri za Lindi na Ruangwa na wananchi wa kijiji cha Nangumbu kwenye uwanja wa shule ya msingi Nangumbu ambako mwenge huo ulipokelewa saa 1:44 asubuhi ukitokea Nyangao wilayani Lindi.

Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Ruangwa, aliwasili wilayani Ruangwa jana jioni, ili kushiriki mbio za mwenge. Kesho (Alhamisi, Oktoba 10) mwenge huo utaelekea Nachingwea, ambapo Ijumaa (Oktoba 11) utaenda Liwale, Jumamosi (Oktoba 12) utaenda Kilwa na Jumapili (Oktoba 13) utakuwa Manispaa ya Lindi ambako utahitimisha mbio hizo na kuzimwa Oktoba 14, mwaka huu.

Waziri Mkuu amewataka wananchi wote wajiandikishe kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili Tanzania iweze kupata viongozi bora. “Tuitikie kaulimbiu ya mwaka huu kwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Hapa Ruangwa, hadi jana jioni watu 28,000 walikuwa tayari wamejiandikisha. Tukachague viongozi wachapakazi na waadilifu watakaoleta maendeleo kwa nchi yetu,” amesisitiza.

Mapema, akizungumza baada ya kupokea mwenge huo saa 2:21 asubuhi, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Hashim Mgandilwa alisema utakimbizwa kwenye kata saba na vijiji 17 ambapo miradi mitatu mikubwa yenye thamani ya sh. bilioni 2.9 itazinduliwa.

Katika kijiji cha Nangumbu, mwenge ulizindua mradi wa mabweni na klabu ya kupiga vita rushwa kwenye shule ye sekondari ya Hawa Mchopa. Ukiwa njiani, mwenge huo ulipitishwa kijiji cha Nandagala ambako Waziri Mkuu alizaliwa. Pia aliupokea na kuukimbiza kidogo akiwa na wanakijiji wenzake, kisha mwenge huo ukaendelea kukimbizwa kuelekea kata ya Likunja ambako watazindua mradi wa maji wa Kitandi. Pia mwenge huo utazindua mradi wa barabara ya lami kwenye kata ya Nachingwea, iliyoko Ruangwa mjini.

 Akizungumza kabla ya kuanza kwa mbio za mwenge wilayani Ruangwa, kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa, Bw. Mzee Ali Mkongea alimshukuru Waziri Mkuu kwa kujumuika na wananchi kushiriki ratiba ya mapokezi ya mwenge wilayani humo.

 Alisema Serikali ya awamu ya tano, ndani ya miaka mitatu (2015-2018) imekamilisha kwa wakati miradi 124 ya maji ambapo aliitaja baadhi yake kuwa ni miradi mikubwa ya Chalinze, Bagamoyo, Arusha, Tabora na Musoma. Pia alisema Serikali imeendelea na uchimbaji wa visima virefu na vifupi vya maji kwa gharama ya sh. bilioni 14.

 “Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzana kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimeingia mkataba na Serikali ya India wa dola za Marekani milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji kwenye miji 28 ya Tanzania. Lakini kuna changamoto nyingi kwenye miradi hii ikiwemo matumizi mabaya ya fedha za umma na wakandarasi kujenga baadhi ya miradi chini ya kiwango.”

 “Pia kumekuwa na shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji. Wananchi tusaidiane kuvilinda vyanzo hivi kwa sababu kazi ya kuvitunza si ya Serikali peke yake bali inaanza na mimi na wewe,” alisema.

 Aliwasihi wananchi hao wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili waweze kuchagua viongozi wazalendo ambao wana calibre ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.

 

Akitoa takwimu za ugonjwa wa malaria nchini, Bw. Mkongea alisema mkoa wa Kigoma unaongoza kwa maambukizi ya ugonjwa huo kwa asilimia 24, ukifuatiwa na Geita (asilimia 17), Mtwara (asilimia 15) na Lindi wenye asilimia 12.  

 

“Niwasihi wananchi tumieni vyandarua vinavyotolewa bure na Serikali hasa akinamama wajawazito na watoto walio na umri chini ya miaka mitano. Kuna maeneo tumekuta baadhi ya watu wakivitumia kuvulia samaki na kufungia bustani ili kuku wasiingie. Haya si matumizi yake hata kidogo,” alisisitiza.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO