Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Waziri Nape : Natoa Siku 14 Mhuishe Tovuti za Serikali

Posted on: May 9th, 2022

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye amewataka Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali kuhuisha  taarifa za Serikali kwenye tovuti za Serikali na mitando ya kijamii ili wananchi waweze kupata taarifa na kujua kinachoendelea kuhusu Serikali yao.


Akizungumza leo jijini Tanga wakati akifungua Kikao cha 17 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali, Waziri Nape amesema kuwa Maafisa Habari wa Serikali ni daraja linalorahisisha mawasiliano kati ya Serikali na wananchi, hivyo ni muhimu kutimiza  wajibu wao kwa kuwa na taarifa sahihi za Serikali na kwa wakati katika tovuti za Wizara au Taasisi zao.


“Natoa siku 14 kuanzia Mei 14 mwezi huu kila tovuti ya Serikali  na mitandao ya kijamii iwe  na taarifa za Serikali zinazoendana na wakati kuhusu utekelezaji wa Sera au miradi mbalimbali ya Serikali, Afisa atakayeshindwa kutekeleza hili tutaachana nae”, amesema Mheshimiwa Nape


Aidha, akiwa katika kikao hicho Waziri Nape ameiagiza Idara ya Habari – MAELEZO kuandaa mfumo utakaowezesha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano nchini kupatiwa mafunzo kuhusu miradi ya kimkakati inayotekelezwa nchini ili waweze kuwa na uelewa na kuweza kuisemea miradi hiyo, kuandaa mfumo wa Maafisa Habari kujadiliana masuala mbalimbali kwa kutumia teknolojia ya kisasa pamoja na kuwa na mfumo wa kupima utendaji kazi wa Maafisa hao.


Katika hatua nyingine, Waziri Nape ameahidi kutatua changamoto ya uhaba wa Maafisa Habari katika ngazi ya Wizara na Halmashauri ili kuhakikisha Serikali ina wataalamu wa kuisemea katika ngazi hizo.


“Nawaahidi hili liko ndani ya uwezo wangu la kusaidia kupata Maafisa habari katika mikoa ya Lindi, Manyara, Mbeya na Tabora na mikoa ya Dodoma, Kigoma na Geita mbayo Maafisa Habari wake wamekuwa Wasaidizi wa Wakuu wa Mikoa. Dodoma.



Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi amesema kuwa Kikao Kazi hicho kitandaa mkakati na kujifunza namna ambavyo dunia itahabarika kupitia Tanzania na kufikisha ujumbe wa maendeleo na namna ya  watu kushiriki katika shughuli za maendeleo.


Pia Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kuwa kuwa lengo la kikao  kazi hico cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini ni  kujengeana uwezo wa namna bora ya kuisemea Serikali na kuwa atahakikisha maagizo yote yaliyotolewa yanatekelezwa ili kutimiza jukumu hilo kwa ufanisi.


Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO