Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Zimbabwe Kuendelea kuimarisha uhusiano na Tanzania

Posted on: June 28th, 2018


Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Emmerson Mnangangwa  amesema serikali yake itaendelea kushirikiana  na kuimarisha uhusiano wake na Tanzania  ili kuimarisha uchumi wa nchi hizo mbili.

Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam leo, Rais Mnangagwa  amesema kuwa Tanzania imesaidia kwa kiasi kikubwa katika harakati za ukombozi wa nchi za Zimbabwe, Afrika  Kusini, Namibia na Msumbiji na hivyo ni jukumu lao kuimarisha uhusiano huo mzuri.

“Sisi kizazi cha zamani ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tunakieleza kizazi cha sasa kuhusu  jitihada za Tanzania katika harakati za ukombozi  wa nchi za kusini mwa Afrika”

“Tulikuwa tunakuja hapa, jengo hili na Mwalimu Nyerere alikuwa Rais wakati huo, ambapo aliweza kusuluhisha migogoro iliyokuwepo kati ya chama cha ZANU na ZAPU” aliongeza Rais Mnangangwa.

Rais Mnangagwa alisema kuwa serikali yake iko tayari kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali yatakayosaidia kukuza uchumi wake na kuahidi kuwa  baada ya Uchaguzi Mkuu kuisha utaotarajiwa kufanyika Julai 30 mwaka huu, Tume ya Ushirikiano itakutana kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo ya kibiashara.

Kwa upande wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alisema Tanzania  na Zimbabwe ni nchi marafiki tangu harakati za uhuru mwaka 1960.

Ambapo  mwaka 1982  ilianzishwa Tume ya pamoja ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zimbabwe  kupitia taasisi mbalimbli za kimataifa ikiwemo SADC.

Aidha, Rais Magufuli ametaja mikakati ya  kukuza na kuimarisha ushirikiano wa uchumi  katika maeneo ya sita ambayo ni   biashara ambapo nchi hizo zimedhamiria kutumia fursa za SADC za kulegeza masharti ya biashara.

Maeneo mengine ni  la kukuza uwekezaji , utalii, usafiri wa anga na barabara, kushirikiana kupitia SADC kwa maana ya fursa za wanachama. Pamoja na eneo la ulinzi, usalama, afya, utamaduni, sanaa na michezo.

Vilevile, Rais Magufuli amesema wanawakaribisha Wazimbabwe kuja kuwekeza nchini Tanzania hasa ukizingatia kwamba kuna kiwango kidogo cha uwekezaji baina ya nchi mbili ambazo ni marafiki wa muda mrefu.

“Mwaka 2006 kiwango cha uwekezaji cha Zimbabwe nchini kilikuwa na thamani ya biashara ya sh. bilioni 18.3, huku mwaka 2017 ikiwa sh. bilioni 21.1, hivyo tumekubaliana kuimarisha baadhi ya maeneo ili kuleta mkakati wa kuimarisha uchumi wa nchi hizi mbili” alisema Rais Magufuli.

Rais Mnangagwa ambaye yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, kesho juni 29 anatarajiwa kutembelea Chuo cha Sanaa cha Kaole Bagamoyo ambacho awali kilitumika kutoa mafunzo kwa wapigania uhuru kutoka nchi za Kusini mwa Bara la Afrika. Ambapo  Rais Mnangagwa ni miongoni mwa waliopata mafunzo katika chuo hicho.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO