Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Afrika ni muhimu kwa Maendeleo ya Uchumi wa Dunia- Putin

Posted on: October 24th, 2019

RAIS wa Urusi, Vladimir Putin amefungua Kongamano la Biashara baina ya Urusi na Afrika (Russia Business Forum) ambapo amesema Bara la Afrika ni muhimu katika maendeleo ya uchumi wa dunia na ni kivutio kikubwa kwa wafanyabiashara wa Urusi.

Ameyasema hayo  Jumatano, Oktoba 23, 2019 wakati akihutubia mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Olympic Park katika mji wa Sochi nchini Urusi. Rais Putin amesema takwimu zilizotolewa na watalaamu wa masuala ya uchumi zinaonyesha kwamba pato la Afrika (GDP) litafikia dola trilioni 29 ifikapo 2050.

Amesema biashara kati ya Urusi na Afrika imeongezeka mara dufu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita na kufikia dola za Marekani bilioni 20 na kwamba nchi yake inaunga mkono wazo la kuanzishwa eneo huru la biashara katika bara la Afrika ukiwa ni mkakati wa Umoja wa Afrika (AU) na kwamba itatoa ushirikiano ili kufanikisha wazo hilo.

Kadhalika, Rais Putin ameongeza kuwa nchi yake inatekeleza kwa vitendo mpango kuzifutia madeni nchi za Afrika na hadi sasa imeshafuta madeni ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 20. 

Amesema utoaji wa mafunzo ya taaluma mbalimbali umekuwa ni utamaduni wa ushirikiano kati ya Urusi na Afrika. “Hadi katikati ya miaka ya 80 nchi yake imejenga taasisi zipatazo 100 za mafunzo mbalimbali Barani Afrika na watu 500,000 wampata mafunzo katika taasisi hizo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameshiriki katika mkutano huo akimwakilisha Rais John Pombe Magufuli. Pamoja naye idadi kubwa ya Wakuu wa Nchi na Serikali katika Bara la Afrika wamehudhuria mkutano huo.

Miongozi mwa viongozi hao ni Rais Yoweli Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais wa Misri na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Abdel Fattah al Sissi, Rais wa Afrika ya Kusini, Cyril Ramaphosa, Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi na viongozi wengine kutoka Bara la Afrika.

Leo Alhamisi, Oktobba 24, 2019 Waziri Mkuu anatarajia kushiriki katika mkutano baina ya Urusi na Wakuu wa nchi na Serikali wa Bara la Afrika. 

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO