Kukusanya, Kuandika na Kusambaza Habari na Taarifa.
Kuhifadhi picha za matukio mbalimbali ya Serikali na Maendeleoya wananchi katika maktaba ya picha.
Kusimamia utoji wa machapisho mbalimbali likiwemo jarida la nchi yetu, Bango na Kijitabu cha Baraza la Mawaziri pamoja na Gazeti la Ukutani la MAELEZO.
Kujibu hoja mbalimbali zinazojitokeza katika vyombo vya Habari.
Kuandaa na kusimamia mikutano ya waandishi wa Habari.
KITENGO CHA USAJILI WA MAGAZETI NA URATIBU WA VYOMBO VYA HABARI
Kazi za sehemu hii ni;
Kusajili magazeti na majarida mbalimbali.
Kufuatilia maudhui ya Habari zinazochapishwa kwenye magazeti na majarida.
Kutoa vitambulisho kwa wanahabari wa ndani na nje ya Nchi.
Kuchapisha kitabu cha anuani za vyombo vya habari(Media Directory)
Kuhakiki orodha ya magazeti yaliyosajiliwa pamoja na wahariri wake.
URATIBU WA MAWASILIANO SERIKALINI.
Kazi za sehemu hii ni;
Kuratibu vitengo vya Habari KATIKA Wizara, Idara, na wakala wa Serikali.
Kukusanya na kuhifadhi Habari na picha kutoka vitengo vya Habari Serikalini.
Kufuatilia utendaji kazi wa Makampuni na Mashirika ya Habari yaliyo chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kama vile TSN na TBC.
Kuandaa mwongozo wa maadili ya Maafisa Habari wa Serikali.
Kuratibu shughuli za Waambata wa Habari katika Balozi za Tanzania nchi za nje.