Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

AG Mpya Aahidi Makubwa Sekta ya Sheria

Posted on: February 3rd, 2018

Na Fatma Salum

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi ameahidi kufanya kazi kwa bidii ili kupunguza changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Sheria hapa nchini.

Akizungumza baada ya kuapishwa katika hafla iliyofanyika leo ikulu jijini Dar es Salaam, Dkt. Kilangi alisema kuwa changamoto hizo haziishii katika ngazi ya kitaifa tu bali hata kwenye nchi nyingine za Afrika na Jumuiya za Kimataifa.

"Natambua kuwa yapo mambo mengi yanahitaji kufanyiwa kazi na kila nchi katika Afrika ikiwemo Sheria za udhibiti wa rasilimali zetu na mfumo wa Sheria za Kimataifa unaohusu masuala ya uwekezaji", alisisitiza Kilangi.

Kilangi aliongeza kuwa atahakikisha ofisi yake inazishughulikia kwa karibu changamoto hizo kwa kushirikiana vyema na wadau wengine wa sheria ili kuongeza ufanisi katika Serikali kwa maslahi ya taifa.

"Tunakuahidi Mhe. Rais kwamba tutafanya kazi kwa akili zetu zote, nguvu zetu zote na uwezo wetu wote kwa maslahi ya Watanzania", alisema Kilangi.

Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma aliwapongeza majaji wapya walioapishwa katika hafla hiyo na kuwaeleza kuwa nafasi ya Majaji wa Mahakama Kuu ni muhimu sana katika taifa hivyo ni wajibu wao kufanya kazi na kufuata sheria bila upendeleo.

Naye Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi alibainisha kuwa mabadiliko aliyofanya Mhe. Rais ya kuwateua Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Naibu wake ni mwanzo tu wa mabadiliko makubwa ambayo amedhamiria kuyafanya katika Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali.

Alieleza kuwa lengo la mabadiliko hayo yanayotekelezwa na Rais John Magufuli ni kuongeza uwajibikaji na ufanisi katika utendaji kazi.

"Namuomba Mhe. Rais taratibu zifanyike ili wanasheria wote walioko katika wizara zote za Serikali Kuu warudi chini ya usimamizi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kuimarisha uwezo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kuongeza ufanisi", alisema Kabudi.

Akitoa nasaha zake kwa wateule walioapishwa kwenye hafla hiyo, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson aliwaasa kutofanya kazi kwa mazowea kwa kuwa yapo mambo mengi yanahitaji maboresho ikizingatiwa kwamba ulimwengu unabadilika kwa kasi kubwa.

Aidha, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju ambaye uteuzi wake ulitenguliwa katikati ya wiki hii ameapishwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na kuahidi kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano katika kuwatumikia wananchi na taifa kwa ujumla.

Katika hafla hiyo iliyohusisha kiapo cha utii na kiapo cha maadili walioapishwa ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi , Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Paul Ngwembe na Majaji wawili wa Mahakama Kuu ambao ni George Masaju na Gerson Mdemu.

Kabla ya uteuzi, Dkt. Adelardus Kilangi alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) kituo cha Arusha na Paul Ngwembe alikuwa Mkurugenzi wa masuala ya Sheria katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA).

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO