Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Bilioni 152 Kutumika Kuunda Meli Mpya ya Kisasa na Kukarabati Meli Chakavu

Posted on: September 3rd, 2018


Serikali imesaini mikataba minne ya miradi ya uundwaji wa meli mpya, chelezo na ukarabati wa meli mbili chakavu yenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 152.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mikataba hiyo iliyofanyika leo mkoani Mwanza, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alisema kuwa miradi hiyo yote itatekelezwa katika bandari ya Ziwa Victoria mkoani humo.

 

“Nimefurahishwa sana na hatua hii ya utiaji saini wa ujenzi wa meli mpya na ukarabati wa meli zilizokuwepo, dhumuni ni kuboresha huduma ya usafiri katika Ziwa Victoria,” alisema Rais Magufuli.

Pia alibainisha kuwa fedha zote za utekelezaji wa miradi hiyo ni fedha za Serikali ya Tanzania zilizopatikana kupitia vyanzo mbalimbali vya kodi hapa nchini.

“Fedha hizi zote ni zetu, Wakorea ni wakandarasi tu,nawaomba Watanzania msikwepe kodi na muamini kuwa fedha mnazozikusanya hazitapotea, tutazisimamia,” alisisitiza Rais Magufuli.

Aidha katika hafla hiyo Rais Magufuli aliahidi kutoa shilingi bilioni 3.7 ndani ya wiki mbili kwa ajili ya kulipa madeni ya mishahara ya wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli, Erick Hamisi alibainisha kuwa  ujenzi wa meli hiyo ya kisasa katika Ziwa Victoria utagharimu shilingi bilioni 88.76 na itakuwa na uwezo wa kubeba tani 400 za mizigo, abiria 1200 na magari madogo 20.

“Meli hii itakuwa kubwa kuliko zote katika Ukanda wa Maziwa Makuu, itakuwa na urefu wa mita 90 na kimo cha mita 10.9 sawa na ghorofa 3 kwenda juu,” alisema Hamisi.

Pia alieleza kuwa ujenzi wa meli hiyo utakamilika katika kipindi cha miezi 24 na itajengwa katika bandari ya Mwanza na mradi huo utatoa ajira kwa watanzania zaidi ya 250.

Aidha Hamisi alisema kuwa miradi mingine ni ujenzi wa chelezo (slipway) itakayotumika kujenga meli mpya katika Ziwa Victoria ambayo itagharimu shilingi bilioni 35.99 na ikikamilika itaweza kubeba meli yenye uzito wa tani 4000 na itatumika kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa meli mbalimbali.

“Pia tumesaini mikataba ya ukarabati mkubwa wa meli 2 za Mv Butiama na Mv Victoria ambao utagharimu shilingi bilioni 27.61,” alisema Hamisi.

Pia Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe alieleza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo ni juhudi za Rais John Magufuli katika kuhakikisha anasimamia vyema makusanyo ya fedha za watanzania.

Naye Balozi Wa Korea Kusini nchini Tanzania, Song Geum Yong alisema kuwa anawapongeza wahusika wote kwa kusaini mkataba wa utekelezaji wa ujenzi wa meli mpya na chelezo.

“Maendeleo haya yote yanatokana na juhudi kubwa zinazofanywa na watanzania wakiongozwa na Rais Dkt. John Magufuli,” alisema Yong.

Miradi yote hiyo itajengwa na wakandarasi kutoka Korea Kusini wakishirikiana na baadhi ya wakandarasi kutoka Tanzania.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO