Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Dkt. Kalemani Ataka Mradi wa Umeme Bonde la Mto Rufiji Kukamilika kwa Wakati

Posted on: February 14th, 2019

Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, RUFIJI

Serikali imetoa wito kwa Wakandarasi kutekeleza Mradi wa kufua Umeme kwa njia ya Maji mto Rufiji( RHPR) kwa uaminifu, wakati na weledi mkubwa

Wito huo umetolewa leo na Waziri wa Nishati Dkt. Merdad Kamemani wakati wa halfa ya makabidhiano ya eneo la ujenzi wa Mradi huo kwa Wakandarasi Arab Contractors- Osman A. Osman & na Elsewedy Electric kutoka Misri.

" Niwaombe wakandarasi wasitoke eneo la mradi kwani miundombinu ipo, tusingependa kugeuka nyuma, mradi huu uwe kielelezo kwa miradi mingine nchini" ameeleza Dkt. Kalemani

Aidha, Waziri Kalemani ametaja manufaa mbalimbali ya Mradi huo ikiwemo uwepo wa umeme wa uhakika na wa kutosha utakaosaidia maendeleo ya uchumi wa viwanda na wananchi kwa ujumla.

"Pia mradi huo utaboresha shughuli za utalii kwasababu ya ukubwa wa bwawa hilo katika ndani ya Tanzania na afrika hivyo kupelekea kuongezeka kwa pato la taifa nchini" ameongeza Dkt. Kalemani.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Arab Contractors Wael Hamdy amempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kutekeleza miradi mbalimbali katika maeneo mengi nchini.

"Mradi huu sio kwa manufaa ya Watanzania au Wamisri tuu bali kwa Waafrika nzima, hivyo nawaahidi hatutawaangusha tutafanyakazi kwa weledi na kumaliza kwa wakati" amesema Hamdy.

Nae Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango imejipanga kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa wakati.

"Watanzania wanajisikia faraja kubwa kuwa sehemu ya uandishi wa historia sahihi kwa taifa letu kwa kutekeleza mradi huu mkubwa hivyo tumpongeze Rais Dkt. John Magufuli kwa maono sahihi kwa watanzania" ameongeza Dkt. Kijaji.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, amesema kuwa ujenzi wa mradi huo utajumuisha bwawa kuu aina ya (Rollar Compacted) lenye uwezo wa kutunza maji takribani mita za ujazo bilioni 34 na kituo cha kufua umeme zenye uwezo wa MW 2,115.

"Pia patajengwa majengo ya ofisi, karakana, makazi, stoo na huduma za jamii kwa ajili ya uendeshaji wa kituo," amesema Dkt. Mwinuka

Dkt. Mwinuka amesema katika utekelezaji wa mradi huo, kutakuwa na Wataalamu wa mradi kwa ajili ya kuangalia ubora wa utendaji kazi wa mkandarasi.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO