Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Dkt Shein: Tutaendelea kuiunga mkono Jumuiya ya kiswahili ya EAC

Posted on: August 31st, 2017

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, viongozi pamoja na wananchi wake wataendelea kuiunga mkono Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa lengo la kuiimarisha lugha ya Kiswahili ambayo inaendelea kujipatia umaarufu mkubwa duniani kote.

 

Dk. Shein aliyasema hayo wakati alipokuwa na mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Profesa Kenneth Linyani Simala, Ikulu Mjini Zanzibar.

Katika Mazungumzo hayo, Dk. Shein alisema kuwa kuna kila sababu ya kuendelea kuiunga mkono Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo kwa hivi sasa Makao makuu yake yapo hapa Zanzibar kwa kutambua kuwa asili na chimbuko la lugha ya Kiswahili ni Zanzibar.

Alieleza kuwa Zanzibar imefarajika kwa kiasi kikubwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya uwamuzi wa makusudi wa kuyaweka makao makuu ya Kamisheni hiyo hapa Zanzibar kwani Zanzibar inahistoria kubwa ya lugha ya Kiswahili.

Alisisitiza kuwa Afika Mashariki ndio wenye Kiswahili hivyo ni jambo la busara kuwepo kwa Kamisheni hiyo ambayo itaendeleza na kukikuza Kiswahili ili kizidi kuimarika.

Dk. Shein alisema kuwa Kiswahili ni lugha tajiri na maarufu sana ulimwenguni hivyo kuna haja ya kuchukua juhudi za makusudi katika kuhakikisha lugha hiyo inazidi kuimarika na kupata mafanikio makubwa zaidi.

Aidha, Dk. Shein alieleza matumaini yake makubwa ya uongozi wa Katibu Mtendaji huyo Profesa Simala katika kuiendeleza na kuiongoza Kamisheni hiyo muhimu kwa nchi za Afrika ya Mashariki.

Sambamba na hayo, Dk. Shein alieleza haja ya kukiimarisha zaidi Kiswahili pamoja na kukipa hadhi yake katika kukizungumza hasa katika mikutano ikiwemo ya Jumuiya hiyo na mengineyo huku akieleza kusikitishwa kwake na baadhi ya mikutano inayowashirikisha wahusika wengi waswahili hapa nchini lakini huendeshwa kwa lugha ya kiengereza kwa kisingizo cha udhamini wa mikutano hiyo.

Dk. Shein alieleza kuwa hali hiyo ni kinyume na nchi nyengine duniani ambazo zinakuza, zinathamini na kuimarisha lugha zao ambazo huzipa kipaumbele kwa kutambua umuhimu wake katika kuzipa hadhi lugha zao.

Kutokana na hali hiyo, Dk. Shein alieleza haja ya kukizungumza Kiswahili ili kizidi kuimarika na kukijengea heshima na hadhi yake kama ilivyo kwa baadhi ya nchi nyengine duniani ambazo hutumia lugha zao kama lugha za taifa ambapo hutumia hata kusomeshea katika vyuo vyao vikiwemo vyuo vikuu.

Nae Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Profesa Kenneth Linyani Simala alitoa shukurani za dhati kwa Dk. Shein kwa juhudi kubwa zilizochukuliwa na Serikali yake anayoiongoza kwa kuipokea Kamisheni hiyo pamoja na kuipa jengo ambalo kwa sasa ndio makao makuu ya Kamisheni hiyo.

Kutokana na juhudi hizo za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na zile za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katibu Mtendaji huyo alieleza kuwa mafanikio makubwa yatapatikana katika kukiimarisha Kiswahili kutokana na mashirikiano hayo.

Aidha, Profesa Simala alimueleza Dk. Shein kuwa Kamisheni hiyo imeweza kukutana na wadau mbali mbali na kuunda mpango mkakati ambao utazinduliwa katika Kongamano la Kiswahili la kwanza linalotarajiwa kufanyika hapa Zanzibar.

Aliongeza kuwa Kongamano hilo linatarajiwa kuwashirikisha wajumbe 150 kutoka nchi wanachama zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na wajumbe kutoka Uturuki, Burundi, DRC Congo, Burundi, Rwanda, Namibia, Wanahabari, wanasiasa na washiriki wadau wengine kutoka nchi mbali mbali duniani.

Alieleza kuwa miongoni wma mambo ambayo wajumbe hao watajifunza ni pamoja na kuijua historia ya Zanzibar na baadae ripoti itatolewa kwa viongozi wa nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mshariki.

Profesa Simala alitumia futsa hiyo kumueleza Rais Dk. Sheinazma ya Kongamano hilo la kwanza la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambalo linatarajiwa kufanyika hapa Zanzibar kwa mara ya kwanza kuanzia tarehe 6 hadi tarehe 8 mwezi ujao.

Sambamba na hayo, Profesa Simala alimueleza Dk. Shein miongoni mwa majukumu ya Kamisheni hiyo kuwa ni kuwaweka pamoja wadau wa lugha hiyo ya Kiswahili huku akieleza kuwa tayari kwa upande wa nchi za nje ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki zimeshatambua umuhimu wa lugha ya Kiswahili ikilinganshwa na nchi husika za Jumuiya hiyo.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO