Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

JPM: Kipaumbele ni Kuhuisha Teknolojia ya Viwanda nchi za SADC

Posted on: August 6th, 2019

Na.Paschal Dotto-MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli amefungua maonesho ya wiki ya viwanda kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Africa (SADC).

Akizungumza katika hafla hiyo ya Wiki ya Viwanda ya SADC jana, Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema kuwa ili kufikia uchumi wa kati viwanda ni kichochea muhimu katika sekta nyingi kwani uwepo wa viwanda utasababisha uhakika wa uzalishaji na uchakataji wa bidhaa na kufanyabiashara kwa nchi wananchama.

Rais Magufuli amezitaka nchi wanachama wa SADC kuweka kipaumbele kwenye kuhuisha teknolojia katika viwanda vilivyoko ndani ya jumuiya ya Maendelea kusini mwa afrika (SADC) pamoja na kushughulikia kwa haraka zaidi vikwazo vinavyochelewesha ukuaji wa viwanda.

“Viwanda ni Sekta muhimu katika kukuza uchumi wa nchi yeyote, kuondoa umasikini, kuongeza ajira na Sekta hii imeziletea Maendeleo makubwa nchi zilizoendelea, kwa hiyo mkutano huu ni dhahiri kuwa sasa nchi za SADC zimeanza kuchukua hatua madhubuti za kukuza sekta hii na ikiwa mkakati huu utatekelezwa utasaidia kukuza uchumi wa nchi zetu”, Rais Magufuli.

Akielezea suala la teknolojia Rais Magufuli amesema kuwa ukuzaji wa teknolojia na ubunifu kwenye sekta ya viwanda ni silaha muhimu kwa nchi za SADC kuendelea na kutegemeana kwani utazalisha ajira, biashara kubwa, na kuepuka kuuza malighafi  kwa wingi nje ya Afrika kama ilivyosasa.

Vilevile,  mchango wa sekta ya viwanda kwa nchi za SADC bado ni mdogo kwani Sekta hiyo inachangia wastani wa asilimia 10 ya pato la taifa na katika Jumuiya ya SADC sekta hiyo muhimu inachangia asilimia 11 tu. Amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alizitaka nchi wanachama wa SADC kujikita zaidi katika kukuza ubunifu na teknolojia rahisi kwenye sekta ya viwanda kwa kuwaendeleza vijana na kuimarisha viwanda vidogo vidogo vilivyoko kwenye jumuiya, kwa hiyo wiki ya viwanda ni fursa muhimu kwa nchi  zote wananchama.

“Wiki ya Viwanda ya SADC ni fursa ya kubadilishana uzoefu miongoni mwa wadau kuhusu utekelezaji wa mikakati ya miaka 49 ya uendelezaji wa viwanda katika jumuiya yetu, bado tunasafari ndefu kuhakikisha sekta ya viwanda inazidi kukua na kuleta mageuzi ya kiuchumi katika nchi zetu”, Amesema Rais Magufuli

Rais Magufuli amesisistiza kwa kusema kuwa katika kuimarisha mashirikiano ndani ya Jumuiya ya Maendeleo (SADC) ni lazima kuimarisha sekta ya uwekezaji kwani nchi hizo zina fursa nyingi kwenye uwekezaji ikiwemo  viwanda vya  madini, kilimo, uvuvi na ufugaji kwa hiyo wananchi kutoka SADC wanatakiwa kuchangamkia fursa kwenye soko la takribani watu milioni 344.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Innocent Bashungwa amesema kuwa uthubutu wa Rais Magufuli kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati wenye viwanda ni mkubwa na  matokea yake  yanaonekana sasa. Hivyo, maonesho haya ni moja ya njia muhimu ya kuimarisha sekta ya viwanda nchini.

“Maonesho haya ya wiki ya viwanda yanawawezesha wanachama wa SADC kuona namna nchi wenyeji inavyotekeleza uwekezaji kwenye sekta ya Viwanda. Aidha,  tunaamini wazalishaji, wafanyabiashara, na wananchi kwa ujumla watachangamkia fursa mbalimbali zitazotokana na mkutano huu wa SADC.”, Waziri Bashungwa.

Waziri Bashungwa alisema kuwa Tanzania inafanya vizuri kwenye biashara ndani ya SADC  kwani takwimu zinaonyesha kuwa mauzo ya Tanzania kwenda SADC mwaka 2018 yalikuwa dola za kimarekani milioni 999 ikilinganishwa na dola za kimarekani milioni 875 mwaka 2017 ikiwa na ongezeko la asilimia 12.16.

Naye Waziri wa Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Amina Ally amesema kuwa uthubutu wa Rais Magufuli wa kuendeleza ndoto ya Baba wa Taifa, Mwl . Julius Nyerere kwa kujenga bwawa Kubwa la kufua na kuzalisha umeme mto Rufiji ni hatua kubwa kwa maendeleo ya sekta ya viwanda.

Balizo Amina alisema kuwa katika utekelezaji wa miradi yote inayofanywa na Serikali suala muhimu ni uwepo wa amani kwa Tanzania na ndiyo maana ikachaguliwa kuwa mwenyeji wa maonesho ya SADC yakifuatiwa na Mkutano mkuu wa viongozi wakuu wa nchi za wanachama wa SADC.

“Tanzania itaendelea kuwa kisiwa cha amani na kwa tukio hili itaendelea kudumisha amani na utilivu kwani mpaka sasa maonesho na mkutano mkuu unaofanyika hapa unaonesha kuwa tanzania ni nchi ya amani”, Waziri wa Viwanda Zanzibar, Amesema Balozi Amina Ally.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt.Stagomena Tax, amesema kuwa juhudi za Serikali ya Tanzania kutekeleza mradi mkubwa wa kufua na kuzalisha umeme mto Rufiji ni moja ya njia madhubuti katika kuimarisha na kukuza sekta ya viwanda kwa Jumuiya ya SADC.

“Kutekelezwa kwa Mradi wa umeme mto rufiji tunaamini kuwa Tanzania itazalisha umeme wa kutosha, tunaomba ziada iweze kwenda kwenye nchi wanachama wa SADC kwani kumekuwa na changamoto ya kubwa mgawo wa umeme na uendeshwaji wa viwanda unahitaji mambo mengi ikiwemo umeme huwezi kuwa na viwanda bila kuwa na umeme unaozalishwa kwa urahisi, kwa hiyo Tanzania imechukuia maamuzi mazuri kuzalisha umeme mto Rufiji.”, Stagomena Tax, Katibu Mtendaji, SADC.

Aidha Dkt.Stagomena aliwaomba watanzania kutumia fursa zilizopo nchi wanachama SADC kwa kuwa ni soko kubwa ambalo linajumuisha nchi 16, ambazo zinawatu wapatao milioni 344 na pato la taifa la pamoja la dola za Marekani milioni 2.5 hivyo ni muhimu kwa watanzania kuzijua fursa hizo na kuzitumia ipasavyo.

Maonesho ya Wiki ya Viwanda yanayofanyika Tanzania kuanzia tarehe 05 mpaka 9 Agosti 2019 na kufatiwa na Mkutano wa wakuu wa nchi 16 wanachama utakaofanyika Agosti 17 na 18,  2019, katika Ukumbi wa Julius Nyerere Dar-es-salaam.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO