• Wasiliana Nasi
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Baruapepe za Watumishi
    • Malalamiko
TANZANIA INFORMATION SERVICES-MAELEZO
TANZANIA INFORMATION SERVICES-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo IDARA YA HABARI-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kumwakilisha Rais mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi SADC

Posted on: August 18th, 2017

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anaondoka nchini leo kwenda Pretoria Africa ya Kusini ambako atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika utakaofanyika Pretoria, Afrika Kusini tarehe 19 na 20 Agosti, 2017.

Mkutano huo utapokea na kujadili ajenda mbalimbali ikiwemo uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa SADC na Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama; Hali ya Michango mbalimbali ya Nchi Wanachama na Kupokea taarifa ya Mwenyekiti anayeondoka wa SADC Organ.

Pia Mkutano utapokea taarifa ya Katibu Mtendaji wa SADC; Kupitia hali ya kiuchumi katika Kanda ya SADC; Kuwasilisha Kaulimbiu ya Mkutano wa SADC; Taarifa kuhusu Mfuko wa Maendeleo wa SADC; Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Viwanda; Kuwezesha Chuo cha Elimu ya Sayansi na Teknolojia; Maombi ya Serikali ya Comoro na Serikali ya Burundi kujiunga na SADC; Utekelezaji wa Mabadiliko ya Kitaasisi ya Umoja wa Afrika na Mkutano wa Mshikamano kati ya SADC na Saharawi ya Magharibi.

Mkutano huo utatanguliwa na Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC Double Troika Summit) tarehe 18 Agosti, 2017 ambao Tanzania itakabidhi nafasi ya uenyekiti kwa mwenyekiti mpya. Double Troika inahusisha nchi wanachama sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji. Katika mkutano huo Mfalme Mswati III wa Swaziland atakuwa ndiye Mwenyekiti. Ajenda kuu katika Mkutano huu ni kupokea na kujadili taarifa kuhusu hali ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama katika Kanda na hasa nchini DR Congo na Lesotho.

Makamu wa Rais amefuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa AfrikaMashariki, Mhe. Balozi Dkt Augustine Mahiga, Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijange, Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Ashatu Kijaji na watendaji wengine waandamizi Serikalini

Makamu wa Rais na ujumbe wake anatarajia kurudi nchini Agosti 21, 2017.

Matangazo

  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Orodha ya Magazeti na Majarida ambayo Hayajahuisha Leseni ya Uchapishaji Serikalini February 05, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Dkt. Kalemani Ataka Mradi wa Umeme Bonde la Mto Rufiji Kukamilika kwa Wakati

    February 14, 2019
  • Rais Magufuli Ang'ara Afrika Kiuchumi, Utawala Bora

    February 05, 2019
  • Taifa Linakwenda Katika Mwelekeo Mzuri-Rais Dkt. Magufuli

    February 05, 2019
  • Rais Magufuli Aagiza Tozo za Madini Ziangaliwe Upya

    January 22, 2019
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Mtaa wa Shaban Robert

S.L.P: 8031 Dar es Salaam

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@habari.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali ya Mwaka 2017/18
  • Tamko la Serikali kuhusu Matumizi ya Picha za Marais Wastaafu katika Sakata la Usafirishaji wa Mchanga wa Madini
  • Hotuba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akifungua mkutano wa 33 wa Jumuiya ya Mitaa Tanzania (ALAT)
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2016 GWF. Haki zote zimehifadhiwa.