RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 12Septemba, 2017 ametembelea hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania(JWTZ) Lugalo, Jijini Dar es Salaam na kumjulia hali Meja Jen.Mstaafu Vincent Mritaba aliyelazwa hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha wakatiakiingia nyumbani kwake Ununio, Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
MejaJen. Mstaafu Mritaba alishambuliwa kwa risasi jana tarehe 11 Septemba, 2017majira ya mchana na kisha kukimbizwa katika hospitali ya Jeshi Lugalo kwa matibabu.
Mkuu wa kituo cha tiba cha hospitali hiyo na daktari bingwa wa magonjwaya moyo BrigediaJenerali Paul Massawe amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa Meja Jen. MstaafuVincent Mritaba anaendelea vizuri baada ya madaktari kufanikiwa kutoa risasi alizopigwamkononi, kiunoni na tumboni.
MejaJen. Mstaafu Mritaba amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumjulia hali na kumuombeadua ili apone haraka.
Mhe.Rais Magufuli aliyeongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jen.Venance Mabeyo piaametembea wodi ya majeruhi na kuwajulia hali wagonjwa wanaotibiwa katika wodi hiyona baadaye akawasalimu wananchi waliofikahospitali hapo kwa ajili ya kupata matibabu.
Mhe.Dkt. Magufuli amewapongeza Madaktari wa hospitali ya Jeshi Lugalo kwa huduma zamatibabu wanazotoa kwa askari na wananchi wengine na amewahakikishia kuwa Serikaliitaendelea kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utekelezajiwa majukumu yao.
Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO