Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Rais Dkt. Magufuli Awataka Viongozi wa Serikali Kutekeleza Majukumu yao kwa Weledi

Posted on: March 4th, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 04 Machi, 2019 amewaapisha Mawaziri 2, Balozi 1 na kushuhudia Naibu Makamishna wa Polisi 5 wakivishwa vyeo vipya vya Kamishna wa Polisi (CP) na kuapishwa kuongoza Kamisheni za Polisi.

Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Mhe. Balozi Dkt. Augustine Phillip Mahiga kuwa Waziri wa Katiba na Sheria na Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Mhe. Hassan Simba Yahya kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia. Mhe. Balozi Simba amechukua nafasi ya Mhe. Balozi Abdulrahman Kaniki ambaye amemaliza muda wake.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro akiwavisha cheo cha Kamishna wa Polisi na kuwaapisha, Naibu Makamishna wa Polisi 5.

Walioapishwa ni CP - Charles Omari Mkumbo ambaye ameteuliwa kuwa Kamishna wa Intelijensia ya Jinai, CP - Liberatus Materu Sabas aliyeteuliwa kuwa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, CP - Shabani Mrai Hiki aliyeteuliwa kuwa Kamishna wa Maabara ya Uchunguzi wa Kisayansi, CP - Leonard Paul Lwabuzala aliyeteuliwa kuwa Kamishna wa Fedha na Lojistiki na CP - Benedict Michael Wakulyamba aliyeteuliwa kuwa Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Utumishi.

Akizungumza katika tukio hilo Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Mawaziri, Balozi na Makamishna wa Polisi kwa kuteuliwa kwao na amewataka kwenda kutekeleza majukumu yao vizuri  ikiwa ni pamoja na kufanya mabadiliko ya kuondoa dosari zilizopo katika maeneo yao ya kazi na kuongeza ufanisi zaidi huku wakiweka mbele maslahi ya Taifa.

Mhe. Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri linayoifanya lakini ametaka lijitafakari juu ya baadhi ya matukio ambayo yanaacha maswali mengi kwa wananchi juu ya hatua zinazochukuliwa na polisi, na ametolea mfano wa tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji, vitendo vya rushwa, Polisi kuhusishwa na magendo, vitendo vya rushwa na dawa za kulevya, pamoja na hatua zinazochukuliwa dhidi ya Maafisa wa Polisi wanaoshindwa kufanya kazi kwa tija.

Mhe. Rais Magufuli amemtaka IGP - Simon Sirro kutosita kuwaondoa Maafisa wa Polisi wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kuteua ama kupendekeza Maafisa wapya wenye uwezo wa kufanya kazi vizuri, na pia ametaka Polisi iondokane na utamaduni wa kuwapeleka Makao Makuu ya Polisi Maafisa ambao wanashindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwenye vituo vya kazi wanavyopangiwa.

Hafla ya kuapishwa kwa Mawaziri, Balozi na Makamishna wa Polisi imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Mawaziri na Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Madhehebu ya Dini na Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani.

Viongozi walioapishwa pia wamekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

04 Machi, 2019

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO