Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Rais Magufuli Aagiza Tozo za Madini Ziangaliwe Upya

Posted on: January 22nd, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewaagiza viongozi wa Wizara ya Madini na Wizara ya Fedha na Mpango kujadiliana na kukubaliana na wadau wa madini kuhusu utaratibu mzuri utakaowezesha kuongezeka kwa mapato yatokanayo na madini yote yanayozalishwa hapa nchini ikiwemo kupendekeza viwango vya tozo za kodi na ushuru vitakavyowavutia wadau kulipa tozo hizo badala ya kukwepa.

Mhe. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 22 Januari, 2019 katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam baada ya kupokea maoni ya wachimbaji wadogo, wafanyabiashara na wadau wengine wa sekta ya madini wanaokutana kwa siku mbili kituo hapo kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yahusuyo madini.

Katika maoni yao wadau hao wa madini wamemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa tozo kubwa na nyingi zilizowekwa katika madini hasa dhahabu zimesababisha wachimbaji wadogo na kati na wafanyabiashara wengi kukwepa kuuza madini yao katika utaratibu rasmi, hali inayosababisha zaidi ya asilimia 90 ya dhahabu inayozalishwa hapa nchini kutoroshwa na hivyo kusababisha Serikali kukosa mapato.

Wamezitaja tozo hizo kuwa ni kodi ya ongezeko la thamani (VAT) inayotozwa kwa asilimia 18, kodi ya zuio ya asilimia 5, kodi ya ukaguzi ya asilimia 1, ushuru wa huduma wa asilimia 0.3, mrahaba wa asilimia 6 na hivyo kufanya jumla ya tozo kuwa asilimia 30.3, na baadaye wanatozwa kodi ya kampuni kwa mwaka ambayo ni asilimia 30 ya faida.

Aidha, wadau hao wameomba wataalamu na viongozi wa madini wawe karibu na wachimbaji ili kujua uhalisia uchimbaji na biashara yake, kutafuta suluhisho la madini yaliyozuiliwa kusafirishwa nje ya nchi kutokana na kukosekana kwa mitambo ya kuchakatia, kupunguza gharama za leseni, kuanzisha vituo vya masoko ya madini, kupata bei elekezi ya madini ya viwanda na ujenzi na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kununua dhahabu.

Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali itakuwa tayari kufanyia kazi mapendekezo ya wadau hao yenye lengo la kuongeza ukusanyaji wa mapato ikiwemo kupeleka Bungeni marekebisho ya sheria zinazohusu tozo za madini ili nchi iweze kunufaika na rasilimali hiyo, tofauti na sasa ambapo utoroshaji wa madini, ukwepaji wa kodi na wizi vinasababisha madini ya Tanzania kuzinufaisha nchi nyingine.

Amemtaka Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko kuhakikisha anachukua hatua za haraka za kufanya mabadiliko katika maeneo yote yaliyoonesha udhaifu ndani ya wizara hiyo ikiwemo kuwaondoa viongozi na wataalamu ambao wamekuwa chanzo cha upotevu wa mapato ya Serikali, kutafuta wawekezaji watakaojenga viwanda vya kuchenjua na kuchakata madini na kuanzisha vituo vya kuuzia madini.

Mhe. Rais Magufuli ametoa siku 30 kwa Waziri Biteko kuhakikisha ukuta wa kuzunguka madini ya Tanzanite wa Mererani unawekewa kamera za ulinzi na vifaa vya ukaguzi kwa wanaoingia na kutoka katika eneo hilo, pamoja na kuondoa sharti linalowataka vijana wenye ajira ndio waruhusiwe kuingia, hali iliyosababisha kuwepo malalamiko kuwa linasababisha vijana wasio na ajira kuingia kwa kuruka ukuta na kuwepo uhaba wa wachimbaji migodini.

Pia amemuagiza Waziri Biteko kuhakikisha maeneo yote ya madini ambayo yanashikiliwa na watu bila kufanyiwa kazi yananyang’anywa ili wapewe wachimbaji ambao wapo tayari kuchimba madini, kwa kutoa kipaumbele kwa wachimbaji wadogo na wa kati ambao wametajwa kufikia Milioni 6.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango, Baadhi ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu, viongozi wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Viongozi wa Dini na viongozi wa vyama vya siasa.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

22 Januari, 2019

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO