Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

RAIS Magufuli aitaka TAKUKURU kutokuwa na kigugumizi.

Posted on: August 29th, 2017

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutokuwa na kigugumizi cha kuchukua hatua pale wanapokuwa na ushahidi dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.

Mhe. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Agosti 28, 2017 alipotembelea na kuzungumza na wafanyakazi wa TAKUKURU katika ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.

“Kuna mambo mengi ya hovyo yanafanyika, tumehakiki pembejeo za ruzuku na kubaini madai ya Shilingi Bilioni 48 ni hewa, tumebaini wafanyakazi hewa zaidi ya 19,500, tumebaini kaya masikini hewa 56,000 zilizopaswa kupata fedha TASAF, tumebaini wanafunzi hewa 5,850 waliotakiwa kupata mkopo, kuna vichwa vya treni 11 vimeletwa bila kuwepo mkataba na mengine mengi, haya yote yanafanyika kwa rushwa, nataka kuwaona mnachukua hatua stahiki”amesema Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli amesema ana imani na TAKUKURU na amewataka wafanyakazi wa taasisi hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia weledi, uzalendo na uadilifu mkubwa na kwamba Serikali itafanyia kazi changamoto zinazowakabili.

Katika mkutano huo Mhe. Rais Magufuli amepokea masuala mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa TAKUKURU na amewaahidi kuwa Serikali itayafanyia kazi ili kuboresha maslahi yao na mazingira ya kazi.

Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Anjellah Kairuki, Katibu Mkuu Dkt. Laurian Ndumbaro na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Valentino Mlowola.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi na wataalamu wanaosimamia utekelezaji wa miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stieglers’ Gorge Hydropower Project), ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) na ujenzi wa barabara mbalimbali nchini, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Katika Mkutano huo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Matogolo Kalemani ametoa taarifa ya maandalizi ya awali ya kuanza kwa ujenzi wa mradi wa umeme wa Stiegler’ Gorge na kwamba zabuni ya kuanza kwa ujenzi huo itatangazwa tarehe 30 Agosti, 2017.

Mhe. Rais Magufuli amesema fedha za kuanza kwa ujenzi wa mradi huo mkubwa utakaozalisha Megawatts 2,100 zitakazoingizwa katika gridi ya Taifa zipo.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO