Na. Fatm Salum
Rais John Pombe Magufuli amewatunuku kamisheni Maafisa wapya 197 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika sherehe zilizofanyika leo ikulu jijini Dar es Salaam.
Maafisa hao wapya wa Jeshi kundi la 62 la mwaka 2017, wamehitimu mafunzo ya kijeshi katika Chuo cha Mafunzo ya Jeshi Monduli kilichopo mkoani Arusha.
Maafisa waliotunikiwa kamisheni wanaume ni 169 na wanawake 28 wakiwemo Maafisa wageni 14 waliotoka nchi za jirani na nchi rafiki na Tanzania.
Aidha katika sherehe hizo Rais Magufuli alikagua gwaride na kutoa zawadi kwa Maafisa waliofaulu vizuri zaidi kwenye kozi mbalimbali wakati wa mafunzo yao.
Chuo cha Mafunzo ya Jeshi Monduli kilianzishwa mwaka 1969 na Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere eneo la Kurasini Jijini Dar es salaam na mwaka 1976 kilihamishiwa wilayani Monduli mkoani Arusha.
Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO