Na Anitha Jonas – WHUSM, Dar es Salaam
02/12/2020.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali asisitiza kufuatilia suala la usambazaji wa Muziki wa katika "digital platform" kwa kushirikiana na wasanii.
Dkt.Abbasi ametoa kauli hiyo Leo jijini Dar es Salaam Salaam alipofanya ziara ya kutembelea Studio ya Konde Gang kwa lengo la kujionea namna wanafanya kazi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukutana na makundi mbalimbali Sanaa nchini.
Akizungumza katika ziara hiyo Dkt. Abbasi alieleza kusikia kilio cha wasanii wengi cha kutaka kuwa na Tuzo za kitaifa ambazo zitasaidia kuongeza hamasa na ubunifu katika uandaaji wa kazi za Sanaa.
" Nitahitaji unitumie zile 'digital platform' za usambazaji na uuzaji wa kazi za Muziki ambazo hazina ofisi hapa nchini ili serikali tuweze kuwasiliana na balozi zetu tuone namna tunaweza kupata ofisi hizo hapa zitakazoendeshwa na wazawa ile muweze kunufaika,"alisema Dkt.Abbasi.
Naye mmiliki wa Lebo ya Konde Gang na Msanii wa Bongo Fleva Rajabu Abdul maarufu kama Harmonize aliomba Serikali kupitia taasisi zake za BASATA na Bodi ya Filamu kuandaa mpango wa kuwa na utaratibu wa kutoa elimu ili kuweza kuwa karibu na wasanii badala ya kuwaita wasanii pale tu wanapotaka kufungia kazi zao.
Pamoja na Harmonize alifafanua umuhimu wa Serikali kujenga "Arts Arena" nchini sababu itasaidia nchi kupata fursa nyingi za kuendesha matamasha makubwa ya Sanaa yakiwemo ya Afrika, ambayo yatasaidia kukuza uchumi wa Taifa.
Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Hakimiliki na Hakishiriki Tanzania Doreen Sinare alitoa wito kwa msanii huyo kujisajili kwa kueleza umuhimu wa kulinda kazi zake kwani gharama za usajili ni ndogo kwani wimbo mmoja unasajiliwa kwa sh. Elfu Moja na cheti ni shilingi elfu kumi na pia usajili huo unafanyika kwa njia ya mtandao.
Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO