Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Tabora Waanza Kunufaika na Mradi wa Maji Ziwa Victoria

Posted on: March 15th, 2020

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

 

Mradi wa maji kutoka ziwa Victoria umeanza kufanya kazi na kuwanufaisha wananchi ambao wamepitiwa na mradi huo katika mkoa wa Tabora, na unatarajiwa kunufaisha wakazi wakazi
Milioni 1.8 utakapokamilika.

 

Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amesema  mradi huo unaogharimu shilingi bilioni 600 utawanufaisha wakazi wa vijiji zaidi ya 90 vilivyopitiwa na bomba la maji.

 

Amefafanua kuwa, maeneo ambayo mradi huo umepitisha bomba la maji hadi kufikia Tabora mjini ni pamoja na Igunga na Nzega. Amesema, kukamilika kwa mradi huo kutaondoa tatizo la upatikanaji wa maji ya uhakika na salama kwa matumizi ya nyumbani na shuhguli nyingine ambazo zinahitaji maji ya uhakika.

 

Dkt. Abbasi amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha Sekta ya maji kwa kuimarisha miundombinu yake ili kutoa huduma ya maji safi na salama mijini na vijijini.  Amefafanua kwamba, hadi sasa jumla ya miradi 875 inatekelezwa sehemu mbalimbali nchini ambapo kati ya hiyo miradi 802 ipo mijini na miradi 73 ipo vijijini. Jumla ya miradi  ya maji 75 ya vijijini imekamilika.

 

Wakati huo huo Dkt. Abbasi amesema kwamba, kutokana na mageuzi makubwa yaliyofanyika katika sekta ya ardhi, hadi kufikia Machi 2020 jumla ya migogoro ya ardhi 10,000 imetatuliwa. Pia, ufanisi katika mifumo ya upimaji na utoaji wa hati umewezesha kukusanya mapato kutoka shilingi bilioni 54.1 mwaka 2014/15 hadi shilingi bilioni 100 mwaka 2018/19.

 

Kuhusu Serikali kuhamia Dodoma, Dkt. Abbasi amesema, hadi sasa jumla ya Watumishi wa Umma 15,361 wa Wizara na Taasisi za Serikali wameshahamia Makao Makuu ya Serikali, Dodoma. Aidha, maandalizi ya awamu ya pili ya ujenzi wa majengo ya ofisi za Serikali na barabara kwa kiwango cha lami kwa urefu wa kilometa 40 katika mji wa Serikali ulioko Mtumba unaendelea.


Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO