Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

WAZIRI MKUU akutana na Rais wa Viwanda vya sukari wa Cuba

Posted on: August 25th, 2017


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirika la Viwanda vya Sukari nchini Cuba, Bw. Francisco Lled, ambaye amekubali kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuongeza uzalishaji wa sukari nchini.

Shirika la Sukari la nchini Cuba lina uwezo wa kuzalisha tani milioni nne za sukati kwa mwaka huku mahitaji ya ndani ni tani 700,000, ambapo kiasi kinachobaki huuzwa nje ya nchi. Kwa sasa shirika hilo linazalisha tani milioni mbili tu katika viwanda vyake 56.

Waziri Mkuu alikutana na Bw. Lled Agosti 24, 2017), wakati alipofanya ziara katika kiwanda cha kuzalisha sukari cha UGB Central Azucarero 30 de Noviembre katika mji wa San Nicola’s de Bari ambacho ni kati ya viwanda 27 vya shirika hilo linalomilikiwa na Serikali ya Cuba kwa asilimia 100.

Katika mazungumzo yao Waziri Mkuu alimshawishi Bw. Lled kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kuzalisha sukari. Alisema kwa sasa Tanzania kuna viwanda vikubwa vitano vya sukari ambavyo uzalishaji wake hautoshelezi mahitaji ya ndani.

Waziri Mkuu alivitaja viwanda hivyo ambavyo ni Mtibwa na Kilombero (Morogoro), Mahonda (Zanzibar), TPC (Kilimanjaro) na Kagera ambavyo vyote vinazalisha jumla ya tani 320,000 za sukari kwa mwaka huku mahitaji yakiwa ni zaidi ya tani 400,000.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi inatarajia kujenga viwanda vitatu vya kuzalisha sukari, ambavyo vitazalisha sukari itakayotosheleza mahitaji na ndani ya nchi na kiasi kitakachosalia kitauzwa nje.

Kwa upande wake Bw. Lled alisema sera za Cuba haziruhusu shirika kwenda kuwekeza nje ya nchi na badala yake wanaruhusiwa kuzisaidia nchi zinazohitaji kujenga viwanda hivyo kwa kutoa ushauri na usimamizi wa ujenzi wa miradi hiyo.

Alisema Shirika lake lipo tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika usimamizi na kutoa ushauri wa ujenzi wa miradi ya viwanda vya kuzalisha sukari na kwamba walishatoa huduma kama hiyo katika nchi mbalimbali zikiwemo Brazil na Bolivia.

Katika hatua nyingine, Bw. Lled alisema mbali na uzalishaji sukari pia shirika hilo kupitia viwanda vyake vya sukari wanazalisha vyakula vya mifugo, asali ambayo inatumika katika viwanda vya kutengeneza vinywaji vikali pamoja nishati ya umeme.

Alisema miwa ya kuzalishia sukari katika viwanda vyao wanaipata kutoka kwenye vikundi vya ushirika wa kulima wa miwa vilivyoko katika mikoa yote nchi nzima kasoro mkoa wa Havana na Pañar del Rio na kwa mkulima mmoja mmoja ambao kwa pamoja hukusanya miwa katika vituo ambavyo hupeleka kiwandani.

Hata hivyo alisema kuwa viwanda vyao vinanunua miwa kwa bei tofauti kulingana na ubora wa miwa na kwamba shirika lao linawasaidia wakulima kwa kuwaelimisha namna bora ya kulima pamoja na kuwaazima mashine za kuvunia wakati wa mavuno. Miwa yote nchini Cuba inavunwa kwa kutumia mashine.


Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO