• Wasiliana Nasi
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Baruapepe za Watumishi
    • Malalamiko
TANZANIA INFORMATION SERVICES-MAELEZO
TANZANIA INFORMATION SERVICES-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo IDARA YA HABARI-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Profile

Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John P. Magufuli alizaliwa  Oktoba 29, 1959 Wilayani Chato Mkoa wa Kagera ambayo hivi sasa ipo Mkoa wa Geita. Dkt. Magufuli amemuoa Mwalimu Janet na wamejaliwa kupata watoto.

Mwaka 1982 hadi 1983 alikuwa Mwalimu Shule ya Sekondari Sengerema akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati na  mnamo mwaka 1989 hadi 1995 alikuwa Mkemia wa Chama cha Ushirika cha Nyanza  (Nyanza Cooperative Union Ltd) Mwanza.

Harakati zake za kisiasa zilianza mwaka 1995 alipogombea kiti cha ubunge katika jimbo la Chato na kuteuliwa kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Ujenzi. Mwaka 2000 Dkt. Magufuli aligombea na kushinda kwa mara ya pili na kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Ujenzi.

Aidha, katika chaguzi za mwaka 2005 na 2010, aliendelea kuwania kiti cha ubunge katika jimbo la Chato na kushinda uchaguzi huo na kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi hadi mwaka 2008 alipohamishiwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambayo aliiongoza hadi mwaka 2010. Mwaka 2010 alipochaguliwa tena kuwa mbunge wa Chato aliteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi.

Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alipata elimu ya msingi  katika shule ya msingi Chato kuanzia mwaka 1967 hadi 1974. Pia alijiunga na elimu ya Sekondari katika shule ya Seminari Katoke-Biharamulo na Lake Sekondari-Mwanza kati ya mwaka 1975 hadi 1978. Aidha, mwaka 1979 hadi 1981 aliendelea na masomo yake ya kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Mkwawa Mkoani Iringa.

Dkt. Magufuli pia alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria akianzia Makutupora, Dodoma (Julai - Desemba 1983), kisha akaenda kambi ya Makuyuni, Arusha (Januari hadi Machi 1984) na akamalizia katika kambi ya Mpwapwa mkoani Dodoma (Machi – Juni 1984). Mwaka 1985 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akisomea Shahada ya Sayansi ya Elimu akibobea kwenye masomo ya Kemia na Hisabati na alihitimu mwaka 1988.

Kati ya mwaka 1991 na 1994 alijiunga na masomo ya Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza na baadaye mwaka 2006-2009 alijiunga na masomo ya Shahada ya Uzamivu ya Kemia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kutokana na taaluma yake  Dkt. Magufuli ameandika vitabu na machapisho mbalimbali.

Matangazo

  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Orodha ya Magazeti na Majarida ambayo Hayajahuisha Leseni ya Uchapishaji Serikalini February 05, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais Magufuli atunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa

    November 21, 2019
  • Rais Magufuli azindua Kitabu cha Maisha binafsi ya Rais Msaafu Benjamin Mkapa

    November 12, 2019
  • Rais Magufuli akutana na viongozi wa AALCO

    October 24, 2019
  • Afrika ni muhimu kwa Maendeleo ya Uchumi wa Dunia- Putin

    October 24, 2019
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: 25 Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@habari.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali ya Mwaka 2017/18
  • Tamko la Serikali kuhusu Matumizi ya Picha za Marais Wastaafu katika Sakata la Usafirishaji wa Mchanga wa Madini
  • Hotuba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akifungua mkutano wa 33 wa Jumuiya ya Mitaa Tanzania (ALAT)
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2019 GWF. Haki zote zimehifadhiwa.