Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

JPM Aitaka Alat Kuongeza Kasi ya Ukusanyaji Mapato

Posted on: October 3rd, 2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka watendaji wa Serikali za Mitaa kusimamia wananchi wao kulipa kodi ili kuimarisha huduma za jamii kwa watanzania kwani kodi itaongeza mapato na kuboresha huduma za jamii.

Akizungumza  leo jijini Dar es Salaam  katika mkutano wa 33 wa Jumuiya  ya Serikali za Mitaa, (ALAT) Rais Magufuli  amesema kuwa ili nchi iweze  kuendelea kiuchumi lazima wananchi wake walipe kodi kwani hicho ni miongoni mwa chanzo muhimu cha mapato ya Serikali kinachoiwezesha kuwapatia wananchi huduma nzuri na bora.

“Tulianza kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kudhibiti ubadhirifu wa fedha za umma, tulibana mianya ya ukwepaji kodi na kuongeza ukusanyaji mapato kutoka bilioni 800 kwa mwezi hadi trilioni 1.3 kwa mwezi” Rais Magufuli alieleza.

Alifafanua kuwa kutokana na ongezeko hilo Serikali sasa inaweza kulipa mishahara kwa wakati huku ikilipa madeni ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo ilikuwa inaidai Serikali shilingi trilioni 1.3 ambapo hadi sasa imeshalipwa shilingi trilioni 1.2.

Rais Magufuli alieleza kuwa katika utendaji kazi wa ALAT mkutano huo ni muhimu kwa serikali anayoiongoza kwani Jumuiya hiyo ni mhimili muhimu wa kuwaunganisha wananchi na serikali yao hivyo  mkutano huo kwa nchi yetu una umuhimu wa kipekee.

“Kwangu mimi mkutano huu ni muhimu sana kwa sababu ALAT ni chombo kinachounganisha mamlaka na wadau wanaohusika na masuala ya Serikali”, alisisitiza Rais Magufuli.

Akibainisha miradi iliyotekelezwa mpaka sasa kutokana na mapato ya wananchi, Rais Magufuli alisema kuwa huduma ya elimu imeboreka zaidi baada ya serikali kuanza utaratibu wa kutoa shilingi bilioni 18 kwa mwezi katika mwaka wa fedha 2015-2016.

Kufuatia hatua hiyo alisema idadi ya watoto waliojiandikisha kuingia darasa la kwanza ilifikia asilimia 95 huku kidato cha kwanza wanafunzi wakiongezeka kwa asilimia 30 ambapo alisisitiza kuwa uwezo huo umetokana na kuimarika kwa ukusanyaji wa mapato.

Rais Magufuli aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa katika kutekeleza mpango wa Serikali ya Awamu ya Tano wa kuimarisha miundombinu, serikali imeshatia saini mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam mpaka Makutupora Dodoma, ambapo kwa awamu ya kwanza itaanzia Dar es Salaam mpaka Morogoro. Mradi huu mkubwa utagharimu kiasi cha fedha za kitanzania shilingi trilioni 7.062 ambazo kwa asilimia 100 ni fedha za serikali kutoka kwa wananchi walipa kodi.

Alitaja miradi mingine kuwa ni upanuzi wa bandari mbalimbali za mizigo zikiwemo bandari za Mtwara bilioni 130, Dar es Salaam bilioni 926.2, Tanga bilioni 16 pamoja na ukarabati wa meli za mizigo katika Ziwa Nyasa na Ziwa Viktoria ambapo pesa zote hizo ni za serikali kwa asilimia 100.

Akijibu risala ya ALAT, Rais Magufuli ameipongeza Jumuiya hiyo na kuwataka wapambane na wasiogope katika kutenda na kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi.

Naye Mwenyekiti wa ALAT, Gulamhafeez Mukadam ameiomba Serikali kutenga na kupeleka kwa wakati ruzuku katika Halmashauri zao ili waongeze ufanisi katika kazi ya kuwatumikia wananchi na kwenda na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Kauli mbiu ya mkutano huo wa 33 ni “Ardhi kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa ni chachu ya maendeleo, Halmashauri zitenge ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vidogo na vikubwa” ambapo Mukadam alisema kuwa kauli mbiu hiyo inakwenda sambamba na sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania ya viwanda.

ALAT ilianzishwa 1984 kwa lengo la kuwakutanisha pamoja watendaji wa Serikali za Mitaa ili waweze kubadilishana uzoiefu masuala ya utendaji kazi.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO