Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

JPM AMTANGAZA JAJI GALEBA KUWA SHUJAA WA KISWAHILI KATIKA SHERIA

Posted on: February 2nd, 2021

“Tusione aibu katika kutumia lugha ya Kiswahili leo nampongeza na kumteua  Jaji wa mahakama  ya Kanda ya Mara,  Jaji Zepharine Nyalugenda Galeba kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania kwa kutumia lugha ya Kiswahili katika kutoa hukumu ya kesi Namba 23 ya mwaka 2020 Rais Magufuli.

 

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema “ Tunashindwa kukitumia Kiswahili kwa sababu  za kukosa utashi na ujasiri lakini pia ni ishara na kasumba ya kupenda vitu vya nje na kudharau vya kwetu kwa msingi huo nimeamua kumteua Mhe. Jaji Galeba Ujaji wa Mahakama wa Rufaa kutokana na uthubutu na ujasiri aliyoonyesha ya kuandika hukumu kwa lugha ya Kiswahili”

Jaji Galeba alitoa hukumu hiyo katika kesi Namba 23 ya mwaka 2020 ya North Mara Gold Mine dhidi ya Gerald Nzumbi iliyoendeshwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mara.

 Rais amesema kuwa “Nimekuteua kwa makusudi  ili Kiswahili ukakiendeleze kwa Majaji wa Mahakama wa Rufaa ili hiki kilichomsaidia kuwa Jaji wa  Mahakama ya Rufaa asikiachie huko kikawa kisingizio cha kupatia kazi, akawe chachu ya Kiswahili kuanza kutumika”.  

 “Mhe. Jaji Kiongozi na Waheshimiwa Majaji, wananchi wanalia kwa hukumu ambazo hawawezi wakazisoma, kutafsiri tu kwenyewe ni lazima walipe pesa, tunatengeneza mateso na machozi kwa wananchi wengi muwaonee huruma Watanzania” alisisitiza Rais Magufuli.

Akionesha umuhimu wa lugha ya Kiswahili amesema kuwa lugha ya Kiswahili inatumika Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), baadhi ya nchi za jirani na Tanzania, vyombo vya habari maarufu duniani, Tanzania Broadcasting Cooperation (TBC) British Broadcasting Cooperation (BBC), DUTCH WELLE (DW) na  Voice of America (VOA). 

Kiswahili kina historia kubwa katika nchi hii na ndio maana Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye ndiye aliyewaunganisha Watanzania  zaidi ya makabila 121 kwa kutumia lugha ya kiswahili hivyo ni lazima tuienzi hii identity yetu .

Lugha ya Kiswahili ni ya 10 duniani na inaongoza katika Afrika na ndio maana mnaona sasa zimeanza kuitikia, kama vile Afrika ya Kusini, Rwanda, Ethiopia na Mabolozi wengi wanaokuja Tanzania wanajifunza na kutumia Kiswahili katika mikutano yetu. Lakini sisi hapa Tanzania tunadharau Kiswahili, Wachina wako zaidi ya bilioni 1.3 wanazungumza lugha yao, Wajerumani wanazungumza lugha yao kwa nini sisi tusizungumze lugha yetu ya  Kiswahili? Aliuliza Rais Magufuli. 

Katika kuthibitisha kuwa Kiswahili kina misamiati ya kutosha Rais amesema kuwa ipo Kamusi inayoweza kutumika katika  mahakama iliyoandikwa na marehemu Profesa S.A.K Mlacha, kwa msaada wa wanasheria nguli, marehemu Jaji  Augustino Ramdhani  na Dkt Harrison Mwakyembe   waliandaa Kamusi ya sheria na bahati nzuri nimebahatika kuiona Kamusi ya sheria tangu mwaka 1999 imeandika  maneno ya Kiswahili na Kiingereza. 

Akiapishwa Jaji Galeba, Rais Magufuli amesema ni ujasiri wake kutumia lugha ya Kiswahili ikifika kwenye mwenendo wa kesi na hukumu inaandikwa kwa Kiingereza. Mahakama ndio mahali pa mwisho pa kutoa haki unapoona mahali ni final mtu ameondoka na hukumu imeandikwa kwa lugha haijui  hii ina maana hawamtendei haki mhusika.

Akitoa mfano wa kutomtendea haki mwananchi wa kawaida Rais Magufuli amesema kuwa mchukue mama wa miaka 80 au baba ambao wengi wao hawakubahatika kwenda shule  na akiwa Mahakama ya Mwanzo kesi yake ikatolewa hukumu kwa lugha ya Kiswahili, anapoona atafute haki mbele zaidi  anaweza kwenda juu tutafuta haki na Majaji na Mahakimu wote wanatumia lugha ya Kiswahili, inapofikia mwisho jaji anaenda kujipinda na kuandika yale mabombastick kwa lugha ya Kiingereza hapa hatumtendei haki.

Ameongeza kuwa, “Umefika wakati wa kufanya mabadiliko makubwa katika mahakama zetu nafahamu yote haya yametokana na mifumo tuliyorithi kutoka kwa wakoloni  kwa kuwa walikuwa wanatumia lugha ya Kiingereza. Pia, wapo Jaji Mwaipopo na Jaji Rumanyika ambao pia nao waliwahi kuandika hukumu kwa lugha ya Kiswahili tunawashukuru sana”. 

Naye, Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesema masuala yanayohusu haki za mtu ni lazima umtangulize Mungu. “Nasema haya kwa sababu kuna maeneo mengi tunatunga sheria nzuri sana lakini inapofika katika ngazi fulani zinageuka kuwa  kichaka cha kutenda maovu huku wanafuata sheria zote na kutoa mfano wa sheria ya manunuzi ambayo uliomba ifanyiwe marekebisho” .

Aidha, amesema kuwa watu wanatumia vibaya taratibu wa sheria kama ulivyotoa mifano katika masuala ya mikopo ya Benki, pia kwa wananchi wanyonge kama wajane,  kwa kutumia taratibu zilezile za sheria, anajua nikifungua mashtaka kwa mjane huyu mara kadhaa na kuyumbisha mjane atakata tamaa na kukosa haki yake kwa kujinufaisha  yeye asiye na haki. 

“Mini binafsi nakubaliana nawe kuwa kutothamini na kutumia lugha ya Kiswahili hakika hili linadhalilisha utaifa wetu kwa kuwa anayeandikiwa hukumu ni mswahili, anayeandika ni mswahili lakini hukumu inatolewa kwa Kiingereza hapa haki  haitendeki”. 

Kwa upande wake Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania Profesa Ibarahim Hamis Juma amesema “Lugha pia ina haki unapotumia lugha ambayo mtu haielewi na kumhukumu ni sehemu ya kutotenda haki, hivyo Mhe. Rais naomba tuwe na jopo kubwa ambalo linahusisha sekta mbalimbali katika kutafsiri ili tunapokuwa mahakamani tusibishane katika tafsiri ya lugha bali tubishane katika haki”

Akimshukuru Mhe Rais, Jaji Galeba amesema “Mhe. Rais leo ni siku kubwa sana kwa maisha yangu na familia yangu ni jambo la kumshukuru Mungu sasa kwa kutujalia kutuumba kama viumbe wa hali ya juu, lakini kututunuku uhai kwa unyenyekevu mkubwa nashukuru kwa kuniheshimisha nafasi ya juu katika Mahakama”. 

“Nakuahidi kuwatumikia wananchi wa nchi hii kwa kutenda haki vile Mungu anataka tutende haki hapa duniani”.

 

 

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO