Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

MAJALIWA: Viongozi wa Dini wawapinge wanaotaka kuvuruga Amani

Posted on: October 2nd, 2017

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba Viongozi wa Jumuiya na Taasisi zote za kidini nchini wahakikishe wanawapiga vita watu wote wanaopanga na kutaka kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini kwa sababu watakwamisha maenendeleo.

Amesema Serikali inaelewa kwamba dini ni miongoni mwa vyanzo muhimu vya maendeleo ya ustaarabu wa mwanadamu kwani inatoa elimu ya maadili mema yenye kuwafanya waumini waepukane na maovu mbalimbali.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo Jumapili Oktoka 01, 2017 wakati akifungua mkutano Mkuu wa mwaka wa 48 wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya uliofanyika katika eneo la Kitonga kata ya Msongola wilayani Ilala, Dar es Salaam.

Amesema kila Mtanzania anatakiwa ahakikishe anadhibiti matukio yote yenye viashiria vya uvunjifu wa amani kwa kutoa taarifa katika mamlaka husika.”Tanzania ni nchi salama na yenye utulivu, hivyo ni lazima wote tushirikiane kuitunza.”

“Napenda niwahakikishieni kuwa Serikali inaunga mkono juhudi za Jumuiya za kidini katika kupiga vita maovu ya kila aina; mathalan utumiaji wa dawa za kulevya, wizi, rushwa, uzinzi ambao husababisha madhara mengi ukiwemo ugonjwa wa UKIMWI.”

Amesema iwapo dini zetu zitatumika vizuri tutaweza kwa haraka sana kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Magufuli la 'Hapa kazi tu' kwani kila mtu ataepuka uzembe na kuwajibika ipasavyo.

Waziri Mkuu amesema ana imani kwamba jumuiya hiyo kama zilivyo taasisi zingine za kidini itaendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii yetu kwa kuwapatia waumini wao na wananchi kwa ujumla elimu na maarifa ya kuboresha tabia zao na maadili yao kiroho.

Amesema amani na utulivu uliopo nchini unatokana na mambo mengi ikiwemo na wananchi kupata ustawi, kuweza kufanya shughuli zao vizuri na kuwa na imani na Serikali yao, ambayo imejiwekea mikakati ya kuhakikisha wananchi hususan wanyonge wanapata faraja ndani ya nchi yao.

Waziri Mkuu amesema mambo yameweza kupatikana baada ya Serikali kupambana na rushwa na ufisadi pamoja na kuimarisha maadili ya watumishi wa umma, ambayo vimekuwa ni vyanzo vya kupotea kwa amani na utulivu katika baadhi ya nchi.

“Serikali imeweka mikakati madhubuti ya kupambana na ufisadi, kupitia mikataba mibovu na kuimarisha maadili ili kujenga imani kwa wananchi, kuondoa migongano na tofauti ya kipato, kuwa na matumizi mazuri ya rasilimali za umma, kuleta tija kwa kuongeza thamani ya huduma na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.”

Awali, Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry amesema Jumuiya hiyo imekuwa ikifanya mikutano kila mwaka kwa lengo la kukumbushana misingi sahihi ya dini tukufu ya kiislam pamoja na kukuza undugu wao.

Sheikh Chaudhry amesema mkutano wa mwaka huu umejumisha watu zaidi ya 4,000 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wageni kutoka nchi za Uingereza, Canada, Rwanda, Uganda, Ujerumani, Kenya, Burundi, Malawi na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Amesema Jumuiya hiyo mbali na masuala ya kidini pia inatoa huduma mbalimbali za kijamii kama elimu, maji na afya kwenye mikoa tofauti tofauti nchini.

 

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO