Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Rais Dkt. John Pombe Magufuli afanya mazungumzo na Rais wa JICA

Posted on: August 21st, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 21 Agosti, 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA),Bwana Shinichi Kitaoka Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Katika Mazungumzo hayo Bw. Kitaoka amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa uongozi mzuri na wa mfano hususani katika kupambana na rushwa na msukumo mkubwa anaoutoa katika maendeleo hususani katika kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Jitihada zinazosaidia kuimarisha uchumi na kuboresha huduma za kijamii na kuahidi kuwa JICA itaendelea kuwa mshirika mkubwa wa maendeleo kwa Tanzania.

Bw. Kitaoka ambaye ni mara yake ya kwanza kuitembelea Tanzania kama Rais wa JICA amemuahidi Rais Dkt Magufuli kuwa miradi yote ya maendeleo ya nyuma na ya sasa inayotekelezwa kwa pamoja kati ya Tanzania na JICA itamalizika kwa wakati ikiwemo mradi wa ujenzi wa barabara za juu (Flyover) wa TAZARA unaoendelea kujengwa hivi sasa,mradi wa ujenzi wa barabara ya Mwenge - Moroco yenye urefu wa kilomita 4 nukta 3 pamoja na mradi wa ujenzi wa daraja la Gerezani.

 “Tumefikia makubaliano mazuri kuhusiana na miradi tunayoendelea kuitekeleza hapa nchini na wananchi watarajie kuona kazi zikifanyika kuanzia mwezi june,mwakani hususani katika ujenzi wa daraja la gerezani na mingineyo”

Kwa upande wake Mhe. Dkt Rais Magufuli amemshukuru Rais huyo wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan Bw. Shinichi Kitaoka kwa uamuzi wake wa kuja Tanzania na amemhakikishia kuwa Tanzania inatambua mchango mkubwa ambao Japan inautoa katika maendeleo ya Tanzania kupitia JICA, na kwamba itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Japan katika masuala mbalimbali.

Mhe. Rais Magufuli ameishukuru JICA kwa kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi jijini Dar es Salaam ikiwemo upanuzi wa barabara ya Mwenge – Morocco, utakaoiwezesha barabara hiyo kuwa na zaidi ya njia nane, ujenzi wa barabara ya TAZARA, ujenzi wa Daraja la Gerezani njia nne, na barabara ya Bendera tatu hadi Kamata.

 “Tunathamini sana mchango unaotolewa na walipa kodi wa Japan kupitia JICA katika kutekeleza miradi ya maendeleo hapa nchini na ninakuomba kuangalia uwezekano wa kufadhili na kujenga miundo mbinu na miradi mbalimbali ya maendeleo katika Makao Makuu ya nchi Dodoma ambako serikali imedhamiria kuhamia huko ili kuweka alama ya urafiki na mahusiano mema yaliyopo kati ya Tanzania na Japan”

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi wa Japan hapa nchini Mhe. Masaharu Yoshida,Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango Doto James, Katibu Mkuu Ujenzi Mhandisi Joseph Nyamhanga na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini Mhandisi Patrick Mfugale.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO