• Wasiliana Nasi
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Baruapepe za Watumishi
    • Malalamiko
Idara ya Habari MAELEZO
Idara ya Habari MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Idara ya Habari MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Tamasha la Serengeti Music and Arts Festival kufanyika Desemba 16,2020

Posted on: December 2nd, 2020

Anitha Jonas – WHUSM, Dar es Salaam
02/12/2020.
 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi amesema kuwa Serikali itafanya Tamasha la Serengeti Music and Art Festival Desemba 26, 2020 litakalofanyika katika uwanja wa uhuru.
 
Dkt. Abbasi ametoa kauli hiyo Leo Desemba 02, 2020 Jijini Dar es Salaam, katika mkutano na wasanii wa tasnia ya filamu ambapo alisisitiza kuwa siku hiyo itakuwa ni maalum kwa ajili ya kusherekea Sanaa za Tanzania,.
 
Akizungumza katika mkutano huo wenye lengo la kujadili mambo ambayo wanatasnia ya filamu wanahitaji Serikali kufanya ili kusaidia tasnia hiyo kukua na kuendelea sanaa, Dkt. Abbasi alieleza kuwa  Mfuko wa Sanaa na Utamaduni ambao utasaidia kutoa mikopo rahisi kwa wasanii na kutoa elimu, upo tayari na hivi karibuni unatarajia kuanza kazi.
 
" Serikali imesikia kilio chenu cha muda mrefu kuhusu changamoto mbalimbali za kupata maeneo ya kufanyia kazi na inampango wa kujenga eneo ambalo litakuwa na vitu vingi ikiwemo sehemu ya kufanya matamasha ya Sanaa “Arts Arena” na tayari ameshapatikana mtaalamu anayechora ramani ya mradi huo na tunatarajia kujenga kituo cha kisasa,"alisema Dkt.Abbasi.
 
Pamoja na hayo kufuatia malalamiko ya baadhi Wasanii wa Filamu wanawake  juu ya unyanyasaji wa kingono kutoka kwa Waandaji wa Filamu wanaume Dkt.Abbasi ameilekeza Bodi ya Filamu Tanzania kufungua dawati la jinsia kusimamia hilo.
 
Naye Msanii wa Sanaa za Maonesho ya Jukwaani Bw.  Ian Mwaisunga  aliomba Serikali kupunguza ada za tozo kwani wamekuwa wakilazimika  kufanya matamasha ya bure bila kuweka kiingilio kutokana na gharama za tozo pale uwanapoweka kiingilio.
 
Halikadhalika Katibu Mkuu Baraza la Sanaa la Taifa Godfrey Muingereza aliahidi kulifanyia kazi suala la kupunguza tozo hizo katika Kanuni zinazofanyiwa marekebisho hivi sasa.
 
 

 

Matangazo

  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Orodha ya Magazeti na Majarida ambayo Hayajahuisha Leseni ya Uchapishaji Serikalini February 05, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Tamasha la Serengeti Music and Arts Festival kufanyika Desemba 16,2020

    December 02, 2020
  • Serikali kutoa suluhu la Mawakala wa Usambazaji wa Muziki katika “Digital Platform”

    December 02, 2020
  • Uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

    November 05, 2020
  • Uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

    November 05, 2020
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: 25 Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@habari.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali ya Mwaka 2017/18
  • Tamko la Serikali kuhusu Matumizi ya Picha za Marais Wastaafu katika Sakata la Usafirishaji wa Mchanga wa Madini
  • Hotuba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akifungua mkutano wa 33 wa Jumuiya ya Mitaa Tanzania (ALAT)
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • MAELEZO PODCASTS 2020

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2019 GWF. Haki zote zimehifadhiwa.