Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Tanzania Kinara Utawala Bora Afrika Mashariki

Posted on: February 7th, 2018

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Orodha ya Hali ya Demokrasia Duniani (2017 Democracy Index) iliyozinduliwa Februari 2,  mwaka huu  na kuchapishwa na  jarida kongwe na mashuhuri duniani la The Economist  imeitaja  Tanzania kuwa nchi ya kwanza katika maswala ya Utawala Bora kwenye  ukanda wa Afrika Mashariki.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi alisema kuwa Tanzania kuwa    nchi ya kwanza kwenye masuala ya Utawala bora imeweza kusaidia ukuaji wa Uchumi wake.

“Utawala Bora ni kigezo muhimu cha ukuaji wa uchumi na hata ustawi wa jamii, kama ambavyo Orodha ya Hali ya Demokrasia Duniani iliyotolewa na  jarida kongwe na mashuhuri duniani la The Economist imeitaja Tanzania ni ya kwanza katika ukanda wa EAC, ikifuatiwa na nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na DRC.

Pia, ripoti ya Foresight Afrika  na taarifa ya  Uchumi ya Benki ya Dunia vyote vimeitaja Tanzania kuwa katika nchi tano Bora za Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi katika mwaka 2018, nchi hizo ni Ghana, Ethiopia, Kodivaa , Senegali na Tanzania”.

Aidha, Dkt. Abbasi alisema kuwa ukuaji huo wa uchumi ni dhamira isiyoyumba ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Magufuli, ikiwa ni   pamoja na kuhakikisha uchumi mkuu unaendelea kujiakisi katika maisha ya watanzania kupitia utoaji wa huduma kwa wananchi na kuboresha sekta mbalimbali.

Katika sekta ya Afya, Dkt. Abbasi alisema kuwa pamoja na ujenzi wa vituo vya afya unaoendelea nchi nzima na uboreshaji wa hospitali, Serikali imetenga  bajeti ya dawa na vifaa tiba kutoka Bilioni 31 mwaka 2015 hadi Bilioni 269. Aidha, bajeti ya sasa imewezesha Serikali kuboresha  usambazaji wa dawa hadi kufikia asilimia 86 ya uhakika wa kupatikana dawa muhimu.

Bajeti hiyo imewezesha  ukarabati wa  wodi 5 za ICU na kuongezwa vitanda kutoka 21 mpaka 75,  kununua  mashine mpya za CT-Scan yenye uwezo mkubwa imenunuliwa katika hospitali ya Muhimbili na Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya fahamu (MOI)  zenye uwezo mkubwa ambapo wastani wa wagonjwa wanaopimwa imepanda kutoka 20 hadi 50 kwa siku.

Vifaa vingine vilivyonunuliwa ni pamoja na mashine 14 za upasuaji (diathermy machines) na mashine za kuchuja damu kwa ajili ya wagonjwa wa figo zipatazo 25 na kuongeza uwezo wa kuhudumia wagonjwa kutoka 68 kwa siku hadi 126.

Uboreshaji huo wa sekta ya afya umeifanya  Muhimbili kuwa hospitali ya kwanza ya umma katika ukanda wa Afrika Mashariki kutoa huduma za juu za kibingwa hasa oparesheni ya kuweka vifaa vya kusaidia kusikia  ambapo watoto 5 waliokuwa awali hawasikii kabisa walifanyiwa oparesheni mwaka jana na kusikia kwa mara ya kwanza katika maisha yao.  Wengine 6 wamefanyiwa wiki iliyopita.

Katika sekta ya Sekta, Msemaji  huyo wa Serikali alisema kuwa lengo la Serikali ni  kufikisha huduma ya maji kwa asilimia 85 vijijini ifikapo mwaka 2020 kutoka asilimia 67.7 mwaka 2015, makao makuu ya mikoa asilimia 95, Dar es Salaam asilimia 95 na  miji mikuu ya wilaya asilimia 90 ifikapo 2020.

 Ambapo hadi sasa kwa ujumla kuna takribani miradi 1,423 imekamilika na kuna vituo vya maji 117,190 vyenye uwezo wa kuhudumia watu milioni 29 sawa na asilimia 79. Katika miaka hii miwili pekee zaidi ya miradi 388 ilikamilishwa.

Dkt. Abbasi, anafafanua kuwa katika usambazaji wa umeme mijini na vijijini kazi imeendelea kwa kasi kubwa. Katika kutekeleza Mradi wa REA III, kiasi cha shilingi bilioni 985.9 zitatumika kuwafikishia wananchi umeme katika programu maalum iliyoanza kutekelezwa.

Alisititiza kuwa, “Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, imedhamiria kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi si tu  kwa maneno bali kwa vitendo, mfano namna ambavyo Serikali imeongeza wigo wa barabara vijijini na mijini, pamoja na kuundwa kwa  wakala maalum (TARURA) ambao utajikita zaidi katika kuharakisha ujenzi wa barabara za vijijini”

Aliongeza kuwa mwaka huu Serikali inakusudia kutekeleza upanuzi wa njia za mwendokasi jijini Dar es Salaam kwenda njia za barabara ya Kilwa kwenda Mbagala yenye urefu wa  kilomita 19 na barabara ya Uhuru kwenda Gongolamboto yenye urefu wa kilomita 23.9.

Aidha, Dkt Abbasi amewakumbusha watanzania  kuwa wazalendo, kuunga mkono jitihada za Serikali kufanya kazi kwa bidii,  kama ambavyo Serikali ya Awamu ya Tano inasisitiza wananchi kufanyakazi ili kuijenga Tanzania uitakayo.

Share this:

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO