Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Tanzania Yaendelea Kung'ara Kimataifa

Posted on: March 2nd, 2020

Na Mwandishi Wetu

Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki na ya nne Afrika kwa kuweka mazingira wezeshi ya ufanyaji biashara ndogondogo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma, Msemaji mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa kidunia Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika Nyanja mbalimbali ambapo katika suala hilo anasema kidunia imekuwa ya 21.

“Taasisi za Kimataifa zinatambua juhudi za Serikali yetu katika kuwaletea wananchi maendeleo, Baadhi ya masuala yaliyofanyika kwa wajasiriamali wadogo ni kupewa vitambulisho maalum vya kuwatambulisha, tozo mbalimbali zimefutwa ili kuwesesha ukuaji wa sekta ya biashara hapa nchini”,Alisistiza Dkt. Abbasi

Akifafanua Dkt. Abbasi amesema kuwa Kituo cha Kimataifa cha Televisheni cha CNBC Africa kimerusha makala maalum inayoonesha mafanikio ya Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo na kuoneshwa na zaidi ya nchi 100 Duniani.

Katika makala hiyo iliyoakisi sekta za utalii, miundombinu, nishati, madini, kilimo na uzalishaji, Dkt. Abbasi amesema kuwa hatua hiyo ni moja ya ishara kuwa Taasisi za Kimataifa zinaendelea kutambua hatua zinazochukiliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Katika hatua nyingine Dkt. Abbasi amesema kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi aliwasilisha ripoti ya Tanzania katika Baraza la Dunia la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu na kusisitiza kuwa Tanzania itaendelea kuheshimu na kulinda haki za binadamu kama ilivyokawaida yake.

“ Haki za Binadamu sio siasa, kama nchi tumeendelea kusisitiza na tutaendelea kuzienzi haki zote za Binadamu kwa maslahi ya watu wote” , alisisitiza Dkt. Abbasi

Tanzania imetajwa kwa nyakati tofauti na Taasisi mbalimbali za Kimataifa kuwa Taifa la kupigiwa mfano kwa namna inavyochukua hatua za kuwaletea wananchi maendeleo, kupiga vita rushwa, kujenga uchumi na ustawi wa wananchi.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO