Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Uchumi wa Tanzania Wazidi Kukua na Kuimarika

Posted on: January 30th, 2020

Na Immaculate Makilika - MAELEZO

Hali ya uchumi wa Tanzania yazidi kuimarika na kukua  kwa asilimia 6.9 ikiwa ni  takwimu za hadi mwezi Septemba 2019, huku lengo likiwa ni kufikia asilimia 7.0% na 7.1% .

Taarifa iliyotolewa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) Januari 20 mwaka huu, inaonesha  kuwa uchumi wa dunia utakua kidogo kutoka asilimia 2.9 hadi asilimia 3.3 kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2019/20.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo jijini Dodoma, kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Serikali, Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi alisema kuwa, huu ni ukuaji mkubwa katika nchi za Afrika Mashariki nyuma ya Rwanda pekee na bado Tanzania ni miongoni mwa nchi za juu kwenye ukanda wa  Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Afrika kwa ujumla.

Dkt. Abbasi alisema kuwa sekta inayoongoza kwa ukuaji wa uchumi ni ujenzi ambayo inachangia asilimia 16, uchimbaji madini na mawe asilimia 13.7, habari na mawasiliano 10.7, maji asilimia 9.1, na usafirishaji na uhifadhi wa mizigo asilimia 9.1.

Aidha, Dkt. Abbasi alisema kuwa, katika kipindi cha miaka mitatu Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwa katika ongezeko la ukusanyaji wa mapato kwa mwezi kutoka shilingi bilioni 850 mwaka 2015 hadi kufikia shilingi trilioni 1.3.

“Leo ninayo furaha kulitangazia rasmi taifa kuwa kutokana na juhudi kubwa zilizofanywa na Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato na Idara nyingine za Serikali, wastani wa mapato ya kodi kwa mwezi kati ya Julai hadi Disemba, mwaka 2019, umepanda na sasa ni shilingi trilioni 1.5 kwa mwezi. Hii kwa sasa ndio rekodi mpya, na ndio habari mpya ya mjini”, alisisitiza Dkt. Abbasi.

Ukusanyaji wa mapato ni moja ya vipaumbele muhimu vya Serikali ya Awamu ya Tano. Huku ikitazamia kujenga uwezo wa ndani wa kujitegemea kifedha na kupunguza kwa kadri inavyowezekana utegemezi kutoka kwa Wadau wa Maendeleo na kuhakikisha kwamba mipango ya kukuza uchumi na kupunguza umaskini inatekelezwa bila kukwama kwa sababu ya ukosefu wa fedha.

 Aidha, azma ya Serikali ya kuifanya Tanzania nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, haiwezi kufikiwa endapo Serikali haitokuwa na uwezo wa kifedha wa kugharamia shughuli mbali mbali za maendeleo.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO