Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Ujenzi wa SGR Waendelea kwa Kasi, Trilioni 2.957 Zatumika hadi Sasa

Posted on: March 2nd, 2020

Na Frank Mvungi- MAELEZO

Serikali imetumia kiasi cha Shilingi Trilioni 2.957 kutekeleza mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) huku kasi ya utekelezaji ikiongezeka.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma , Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo unaendelea kama ulivyopangwa.

“Mradi wa SGR kwa kipande cha Dar es Salaam na Morogoro umefikia asilimia asilimia 75 wakati kipande cha Morogoro Makutopora Singida kimefikia takribani asilimia 28”, Alisisitiza Dkt. Abbasi

Akifafanua Dkt. Abbasi amesema kuwa watanzania wataanza kutumia usafiri huo wa kisasa kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro mwaka huu wa 2020 hivyo ile ahadi ya Serikali kwa wananchi itatimia kama ilivyopangwa na kwa wakati.

Kwa upande wa kipande cha Mwanza-Isaka Dkt.Abbasi amesema kuwa wakati wowote tenda itatangazwa ili kumpata mkandarasi atakayejenga reli hiyo kwa kipande hicho ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa mwezi Desemba 2019 Jijini Mwanza kwa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano.
Akizungumzia baadhi ya wanasiasa wanaobeza juhudi za Serikali kuwaletea wananchi maendeleo kupitia miradi kama SGR Dkt. Abbasi amesema kuwa Serikali haitarudi nyuma katika kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuwa hata wanaobeza watanufaika na miradi hiyo ikiwemo ndege na umeme.
Kwa upande wa utekelezaji wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere(JNHPP) , ujenzi wa eneo la kuchepusha maji ya mto Rufiji ili ujenzi wa ukuta wa bwawa uanze limekamilika kwa asilimia mia moja, Aidha bwawa hilo linatajwa kuwa kati ya mabwawa makubwa 70 ya kuzalisha umeme wa maji Duniani na kwa Afrika litakuwa la nne kwa ukubwa.
Kwa upande wa kiwango cha fedha kilicholipwa hadi hasa Dkt. Abbasi amesema kuwa Shilingi Trilioni 1.275 kati ya Trilioni 6.5 zimeshalipwa ambapo kazi zote zinaendelea kama ilivyopangwa.
Katika hatua nyingine Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara zote kesho Machi 2, 2020 na watatembelea mradi wa SGR ili kujionea utekelezaji wake.

Akizungumzia utekelezaji wa mradi wa Chelezo katika Ziwa Victoria Dkt. Abbasi amesema kuwa umekamilika kwa asilimia 100 na Shilingi Bilioni 32.8 zimeshalipwa na katikati ya mwezi Machi Itaanza kufanya kazi , huku ukarabati wa MV Victoria umefikia asilimia 89 na Bilioni 14 zimeshalipwa, Wakati MV Butiama ukarabati wake umefikia asilimia 86 na Bilioni 3 zimeshalipwa kati ya Bilioni 4 zilizotengwa kwa ajili ya mradi huo.
“ Ujenzi wa meli mpya na ya kisasa katika Ziwa Victoria itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 1200 na Tani 400 za mizigo umefikia asilimia 52 hadi sasa na unaendelea kutekelezwa kwa kasi kama ilivyopangwa.
Utaratibu wa Msemaji Mkuu wa Serikali kukutana na vyombo vya habari unalenga kuileta Serikali kwa pamoja na wananchi kwa kueleza utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa maslahi yao katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO