Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Ushirikiano wa Tanzania na Kenya Wazidi Kushamili, Mamilioni na Dhahabu Yarejeshwa.

Posted on: July 24th, 2019

Na: Waandishi wetu – MAELEZO DAR ES SALAAM

Rais Dkt. John Magufuli aipongeza Serikali ya Kenya kwa maamuzi yake ya kuirejeshea dhahabu zenye uzito wa kilo 35.34 zilizotoroshwa nchini Tanzania na Wafanyabiashara wasio waamini kwa njia ya magendo mwaka 2018.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi dhahabu pamoja na fedha taslimu akiwa pamoja na ujumbe wa Mawaziri na Watendaji wa Serikali ya Kenya leo Jumatano (Julai 24, 2019) Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema kitendo kilichofanywa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ni cha kizalendo na kimedhirisha urafiki na undugu wa kweli baina yake na Tanzania.

Amesema kuwa  Serikali ya Kenya kupita vya vyombo ulinzi na usalama vimefanya kazi nzuri inayodhirisha ushirikiano uliopo  kati ya Tanzania na Kenya,  na ameeleza kuwa  kama kusingekuwepo na ushirikiano huo dhahabu na pesa  hizo zilizokamatwa kwenye uwanja wa Jommo Kenyatta nchini humo visingelejeshwa Tanzania.

“Tunaipongeza  Serikali ya Kenya kupitia vyombo vya vyake vya ulinzi vilivyofanya kazi nzuri ya kukamata dhahabu kilo 35.34 iliyokuwa imeshavuka kwenye mipaka yetu, na  tuwapongeze pia kwa kutunza pesa yetu ambayo ilibiwa Tanzania kwenye Benki ya NMB mwaka 2004, kwa kweli huu ni uaminifu mkubwa” amesema Rais Magufuli

Licha ya kuipongeza vyombo vya ulinzi vya Kenya Rais Magufuli ameshangazwa na ukimya  kutaka vyombo vya ulinzi vya Tanzania na hivyo kuvitaka kujitafakari kwa namna dhahabu hiyo ilivyoweza kukamatiwa  Kenya na Sio Kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza  ambapo watuhumiwa walitumia ndege ya ‘Precision Air’ kusafirisha mzigo huo.

“Vyombo vyetu vya ulinzi vipo hapa lazima niviseme, dhahabu iliwezaje kufika Kenya tukashindwa kuwakamata watumiwa wakiwa bado kwenye uwanja wa Mwanza?, hapa lazima vyombo vyetu mjitafakari japo mnafanya kazi kubwa lakini ikiwezekana mkajifunze kwa wenzenu wawape mbinu walizozitumia katika hili” amesema Rais Magufuli.

Katika hafla hiyo, Rais Magufuli pia  alimpigia simu ya moja kwa moja Rais Uhuru Kenyatta na kutoa shukrani zake na kumdhibitishia kuwa amepokea mzigo huo na kumpongeza kwa ushirikiano wa Serikali yake kwa Watanzania, ambapo Rais Kenyatta akimuhakikishia Rais Magufuli ushirikiano wa kudumu ambao utachochea zaidi maendeleo kama walivyohaidi na kupewa mamlaka na wananchi.

Naye mjumbe maalumu aliyemwakilisha Rais Kenyatta, Monica Juma ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Kenya amesema Serikali ya Kenya itaendeleza ushirikiano wake na Tanzania katika masuala ya ulinzi na usalama kwa kuwa ushirikiano huo utasaidia kukuza uchumi wa pande zote mbili.

Na kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Palamagamba Kabudi amesema Kenya na Tanzania ni ndugu tokea ezi na enzi, hivyo Serikali Tanzania itahakikisha kuwa inaendelea kushirikiana na Kenya ili kufanya ushirikiano huo unaleta manufaa kwa wananchi wa nchi hizo.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO