Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Waziri Mkuu Awataka Maafisa Mawasiliano Kuyatangaza Mageuzi Yanayoendelea Nchini.

Posted on: March 18th, 2019

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungau Mkutano wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Machi 18, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungau Mkutano wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Machi 18, 2019.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano Serikalini  kuyatangaza na kuyatetea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano  yanayoendelea nchini.

 Pia, amewataka Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano Serikalini kuhakikisha wanatumia vizuri taaluma zao na nyezo wanazopatiwa kueleza mambo yanayofanywa kwenye sekta zote na wasipofanya hivyo watatoa fursa kwa taarifa zinazosemwa na wapinga maendeleo kuonekana kuwa ni kweli.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo katika ufunguzi wa Kikao Kazi cha 15 cha Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano Serikalini, kinachofanyika katika ukumbi wa BOT jijini Mwanza. Kikao hicho kinahudhuriwa na Maafisa Habari na Mawasiliano takbaribani 400.

Amesema maafisa hao wanatakiwa wakumbuke kuwa wanapaswa kuueleza umma wa Watanzania kwa kina masuala yanayofanywa na Serikali hususan katika kipindi hiki ambacho Serikali inatekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/2017 – 2020/2021) wenye kuweka msisitizo kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda.

“Mkumbuke kuwa kazi ya utoaji taarifa kwa wananchi kwa sasa si utashi binafsi wa mtoa habari bali hainabudi kufanywa kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi. Mathalan Sheria mpya ya Haki ya Kupata Taarifa Na. 12 ya mwaka 2016 yenye kuzitaka mamlaka za umma kuwapa wananchi taarifa zinazowahusu”.

Waziri Mkuu amesema sheria hiyo, inakwenda sambamba na sheria nyingine ya kumlinda mwananchi asilishwe taarifa za uongo, uchochezi na uzushi yaani Sheria ya Huduma za Habari Na. 12 ya mwaka 2016.

 

Amesema lengo la katiba na sheria hizo mbili, pamoja na mambo mengine, ni kuwahakikishia wananchi haki ya kupata habari tena zilizothibitishwa kwa maana ya usahihi wake na kwa wakati. “Sababu hizo, ndizo zilizofanya niguswe sana na kauli mbiu yenu isemayo: “utoaji habari sahihi na kwa wakati ni chachu katika kuifikia Tanzania ya kipato cha kati”.

Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kupongeza kazi nzuri zinazofanywa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hususan Idara yake ya Habari – MAELEZO) na timu za habari za viongozi wakuu kama Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na watendaji wengine.

Pia, Waziri Mkuu amesema ameguswa na baadhi ya mada ambazo zitajadiliwa katika kikao kazi hiko, ikiwemo ya namna ya kushughulikia habari za uongo, kutunga, kughushi na namna kada yao inavyoweza kusaidia kukidhibiti kichochoro hicho haramu katika habari. 

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka viongozi na watendaji wote wa taasisi za umma, kuanzia sasa washirikiane na maafisa wa habari kwenye maeneo yao kuhakikisha kuwa habari muhimu kwa wananchi hazizuiwi kwa urasimu kama hazijazuiwa kisheria. Habari zitolewe kwa haraka na kwa njia anuai za kisasa.

Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe afuatilie kuhusu uzinduzi wa tovuti za Halmashauri walioufanya jijini Dodoma tarehe 27 Machi 2017, kama zinafanya kazi ipasavyo.

Amesema lengo la tovuti hizo ni kuiongezea Serikali uwezo wa kuwapatia wananchi habari na taarifa kwa haraka kwa kuzingatia kwamba wako katika kipindi muhimu cha mageuzi katika historia ya nchi, ambapo mambo mengi yanafanyika Serikalini ya kiuchumi na kijamii lakini hayafikishwi kwa wananchi.

“Kuhusu hili, naiagiza Wizara ya Habari kufanya tathmini ya mara kwa mara na kuniletea taarifa kuhusu utekelezaji wa majukumu yenu na matakwa haya ya kisheria miongoni mwa wizara, taasisi za umma na sekretarieti za mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini”.

Waziri Mkuu amesema maafisa hao wanapaswa kufahamu kikao chao kimekuja wakati muafaka kwani Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, ipo katika mwaka wake wa nne wa kutekeleza mageuzi makubwa katika kila sekta zikiwemo za kiuchumi na kijamii nchini.

Amesema katika kipindi cha zaidi ya miaka mitatu kazi kubwa tena ya kihistoria imefanywa na Serikali ya awamu ya tano na wao ni mashahidi wa hayo yanayofanywa. “Ni jukumu lenu sasa kuuhabarisha umma wa Watanzania kama ambavyo Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyotaka katika Ibara ya 18(d).

Waziri Mkuu ametaja mapinduzi makubwa yaliyofanyika kwenye kila sekta nchini ikiwemo elimu; afya; nishati; mifugo; viwanda; barabara; viwanja vya ndege; uchukuzi wa anga; uchukuzi wa reli; uchukuzi wa majini; madini; sanaa za filamu na muziki; utalii na michezo mbalimbali. Amesema maafisa hao wanapaswa kuyatangaza mageuzi hayo.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO