Idara ya Habari-MAELEZO
Idara ya Habari-MAELEZO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Idara ya Habari-MAELEZO

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Idara ya Habari
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Watumishi wa Idara
    • Muundo wa Idara
    • Vitengo
  • Huduma zetu
    • Ukumbi wa Mikutano
    • Taratibu za leseni
    • Kitambulisho cha Mwanahabari
    • Tozo za Huduma
  • Machapisho
    • Sheria
    • Kanuni
    • Fomu
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha za Mnato
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoanza
    • Miradi Ijayo
  • Dawati la Matangazo

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga Azindua Minada ya Kahawa Kanda ya Mbeya /Songwe

Posted on: August 22nd, 2019

Serikali imewataka wakulima wote nchini kwa kupitia vyama vya Ushirika kuweka mkakati wa kununua na kutumia mitambo ya kuchakata kahawa ili kuongeza na kuwa na mwendelezo (Consistency) wa ubora wa kahawa inayozalishwa ili kupata bei nzuri mnadani au kwenye soko la moja kwa moja.  


Waziri wa Kilimo amesema hayo Leo tarehe 22 Agosti 2019 wakati wa uzinduzi wa minada ya kahawa kanda ya Mbeya-Songwe na kuzitaka Halmashauri kupitia vyanzo vyake vya mapato kuendelea kuwekeza katika uendelezaji wa zao la kahawa ikiwemo uzalishaji wa miche, ununuzi wa CPU na kuwawezesha wakulima na maafisa ugani kupata mafunzo ya kilimo bora cha kahawa ikiwa ni pamoja na kuwapatia vitendea kazi.


Alisema kuwa ili kulinda ubora wa kahawa, matumizi ya mitambo ya kisasa ya kuchakata kahawa (CPU) hayawezi kuepukika. Alisema nchini kuna takribani mitambo 481 kiasi ambacho bado kipo chini ukilinganisha na kiasi cha kahawa inayozalishwa. "Hivyo nawasihi wadau wote muone umuhimu wa uwepo wa mitambo hii kwa kuwa ili upate kahawa nyingi zenye sifa za ubora unaofanana ni lazima kuwepo na matumizi makubwa ya CPU tena kwa kuzingatia hatua zote za uchakataji wa kahawa" Alikaririwa Mhe Hasunga.


Mhe Hasunga aliongeza kuwa Lengo la Serikali ni kuona kwamba kahawa zote zinaandaliwa katika mitambo ya kisasa (CPU) ili zipate bei nzuri katika masoko kwani dhamira ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ni kuimarisha tija katika uzalishaji kadhalika kutafuta masoko ya mazao nje na ndani ya nchi.
Alisema kuwa Ili kuhakikisha tasnia ya kahawa inaondokana na changamoto ya tija ndogo na uzalishaji, Serikali kwa kushirikiana na Wadau imeendelea kuchukua hatua mbalimbali zikiwemo kuongeza kasi ya upatikanaji wa miche bora ya kahawa kupitia TACRI; Ruzuku ya miche inayotolewa na Bodi ya Kahawa na kuanzisha utaratibu wa upatikanaji wa mikopo ya mbolea kwa wakati kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Sekta Binafsi.  

Aliongeza kuwa hatua hizo zimewezesha kuongezeka kwa uzalishaji wa kahawa kutoka tani 43,625 za kahawa safi msimu wa mwaka 2017/2018 mpaka kufikia tani 68,147 msimu 2018/2019.


Waziri huyo wa kilimo Mhe Hasunga alisema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa tija katika uzalishaji wa kahawa kwa wakulima wadogo wa kahawa ni ndogo sana ukilinganisha na wakulima wa mashamba makubwa na wakulima wa kahawa wa nchi nyingine. 


Aliongeza kuwa Wastani wa tija kwa mti mmoja wa kahawa ya Arabika ni gramu 350 ikilinganishwa na kilo moja (gramu 1,000) kwa nzi za Brazil na Vietnam. 


Aliziraja Sababu kubwa zinazosabisha tija ndogo kwenye kahawa kuwa ni pamoja na Matumizi madogo ya mbolea na virutubisho kwa ajili ya kuongeza tija na uzalishaji; na Wakulima kutokuzingatia kanuni za kilimo bora cha kahawa ambapo wakulima wengine hawatunzi kabisa miti yao ya kahawa na huvuna tu kile kitakachopatikana.


Sababu nyingine ni Uwepo wa magonjwa na wadudu waharibifu wa kahawa Miti iliyozeeka sana na kupoteza uwezo wa kuzaa vizuri; Badala ya kutumia miti iliyoboreshwa yenye uwezo mkubwa wa kuvumilia magonjwa na kuzaa sana. Nimeambiwa mti wa mmoja ulioboreshwa unao uwezo wa kuzaa wastani wa kilo 3 – 5 za kahawa kavu (Parchment). 


Aidha, Mhe Hasunga amsema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati kuleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya kahawa na kuhakikisha inaendelea kutoa mchango mkubwa katika kupunguza umaskini, kuongeza pato la taifa na kuongeza ajira kupitia viwanda mbalimbali vya kahawa.   


Moja ya lengo kuu la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuijenga Tanzania kuwa nchi ya viwanda.  Ili kufikia lengo hilo, Serikali kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali imeendelea kuhamasisha matumizi ya miche bora ya kahawa ili kuongeza uzalishaji na tija kwa wakulima, kuimarisha mazingira ya biashara na kutatua changamoto zinazoikabili tasnia ya kahawa ili kuiwezesha kutoa mchango unaohitajika katika kujenga Tanzania ya viwanda. 

 
Kuanza kwa minada ya kanda ya kahawa ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuwa kuanzia msimu wa kahawa 2019/2020 Bodi ya Kahawa ianze kuendesha minada ya kahawa katika Kanda nne (4) za uzalishaji wa kahawa. Kanda hizo ambazo minada ya kanda itafanyika ni Kanda ya Mbeya/Songwe mnada unafanyika Mbozi, Kanda ya Ruvuma/ Njombe mnada unafanyika Mbinga Mkoani Ruvuma, Kanda ya ziwa mnada unafanyika Bukoba Mkoani Kagera na Kanda ya Kaskazini  mnada unafanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Matangazo

  • Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari May 03, 2023
  • Baraza la Mawaziri April 14, 2023
  • Uzinduzi wa ‘The Royal Tour’ katika Ukumbi wa Guggenheim uliopo Manhattan, Jijini New York nchini Marekani April 19, 2022
  • Launch of 2019 SADC Media Awards February 13, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisaini nakala 3 za Sheria za Tanzania zilizofanyiwa urekebu kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya urekebu wa sheria, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 23 Aprili, 2025.

    April 23, 2025
  • The Global Goalkeepers Award

    February 04, 2025
  • Mkutano wa Tatu wa Nchi zinazozalisha Kahawa Barani Afrika

    January 28, 2025
  • Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Masuala Nishati

    January 28, 2025
  • Angalia zote

Wasiliana Nasi

Makole, Uhindini

S.L.P: S.L.P 677, Dodoma

Simu: +255-22-2771005

Nukushi:

Email: maelezo@mawasiliano.go.tz

Simu ya Kiganjani:

Kiunganishi cha Haraka

  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari
  • Kanuni za Sheria za Huduma za Habari za Mwaka 2017
  • Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
  • Fomu ya Kitambulisho cha Mwanahabari aliyopo nje ya Tanzania
  • Maelezo Podcasts (Apple Podcasts)
  • Maelezo Podcasts (Spotify)
  • Maelezo Podcasts (Amazon Music)
  • Tanzania 'THE ROYAL TOUR'
  • Tanzania 'The Royal Tour' AMAZON
  • HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
  • Baraza la Mawaziri
  • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UN) TAREHE 23 SEPTEMBA, 2021 JIJINI NEW YORK, NCHINI MAREKANI
  • NCHI YETU - MIAKA 61 YA UHURU
  • NCHI YETU - Miaka Miwili na Samia
  • Mjadala maalum kuhusu mpango wa uwekezaji katika Bandari zetu!

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Zanzibar
  • Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais
  • Tovuti ya Rais-IKULU
  • Southern African Development Community
  • Tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Video za Hivi Karibuni

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2023 Habari - MAELEZO